Sunday, March 16, 2014
KWANINI UENDE UGENINI BILA TAARIFA ?
' Kwanini Uende Ugenini Bila Taarifa ? ', Tutafakari pamoja
Kwa wasomaji na watazamaji wapya karibuni tena leo katika mfurulizo wa koramu hii ambayo inatoka kila siku katika Mtandao huu wa Umojamatukio Blog (UmB) ikiwa na ujumbe tufauti kulingana na jambo linalotokea au linaloweza kutokea na kusababisha kero kwa jamii husika.
Kauri yetu leo Tutafakari pamoja.
' Kwanini Uende Ugenini bila Taarifa ' ?.
Ndugu zangu poleni kwa mambo mengi yaliyowazunguka katika utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku Kitaifa, kifamilia na kibinafsi tafakari yetu leo ni kama kinavyoonesha kichwa cha habari hapo juu (Head line) ' Kwanini Uende Ugenini Bila Taarifa ?' karibuni
Pamoja na tabia nyingine ambazo ambazo ni kero kwa jamii zetu tunazozungumzia katika kurasa au koramu hii hatuwezi kusahau kero hii inayotajwa leo katika ukurasa huu.
Kumezuka tabia kwa baadhi ya watu kujisahau au kwa makusudi kuwasumbua watu wengine katika familia kama nilivyobaisha kwa makusudi au kwa kutokutambua kasoro hiyo kwa wahusika kutokana na baadhi yao kukurupuka kusafiri kutoka upande mmoja wa makazi kwenda katika eneo jingine iwe kwa rafiki ndugu au jamaa bila taarifa ya aina yo yote ikiwa na barua simu au kuagiza kwa mtu aliyekaribu ili mwenye dhamana ya kumpokea mgeni ajiandae ki hali na mali.
Mtu mzima na akili zake timamu anakurupuka kwenda kwa watu anaoamini ni jamaa zake bila taarifa hali inayosababisha kizaa zaa kwa mwenyeji ambaye atalazimika kumhifadhi mgeni huyo katika mazingira ya dharura isiyo ya lazima ambayo pia inaweza kusababisha aibu au usumbufu usio wa lazima kwa mhusika.
Ninasema hivyo kwa sababu najua mazingira ya maisha si mjini tu hata kijijini yahitaji kuwe na utaratibu ili nidhamu ya m,aisha iwepo haikubariki mtu mwenye uelewa unatoka huko iwe nmbali au karibu ufike nyumbani kwa mtu kama mvamizi kwa kutokutoa taarifa ya mapema ili mwenyeji ajiandae unakuwa na lengo gani ? kwa mwenyeji aaibike au afedheheke na akikutolea nje utamuona mbaya.
Juzi wakati nimeketi katika eneo moja la mapumziko nilishtushwa na kauri na mmoja wetu aliyeonekana kuchoshwa na ugeni usio na utaratibu ambao ulikuwa ukimnyima raha kutokana na mvurugano huku akieleza kuwa kuna wageni 5 !!! na familia yake 6 nyumbani katika jiji hili la Dar 'Bongo' unaishije na watu ? !!, huku hao wageni haijulikani wana mipango gani hapa jijini na hajui hatma yao.
Mfano katika maisha ya mijini hivi sasa tofauti na zamani ambapo ilikuwa si jambo la ajabu kumpeleka mgeni kwa ndugu au jirani akalala lakini hivi sasa utapata wapi msaada huo ? , Pia tujiulize ni nani katika maisha ya kada ya kawaida mwenye uwezo wa kuacha chumba kitupu maalumu kwa wageni katika maisha ya sasa ?
Nauliza tena na wewe jiulize 'Kwanini Uende Ugenini bila Taarifa' Tutafakari pamoja tujirekebishe,
Pia tatizo linalofanana na hilo ni kwa baadhi yetu katika jamii kutembelea nyumba za watu na kupiga kambi zisizo na tija huku tukileta story za uvumi na uongo ili kusogeza muda wa riziki hii nayo ijadiliwe ikibidi tabia hii iachwe kwani inaweza kuchangia kuvurugika kwa maisha ikiwa ni pamoja na kuvunjika kwa ndoa maana penye wengi pana mengi. Tutafakari pamoja Tujirekebishe.
Haikubariki mtu utoke kusikojulikana au hata kama kunajulikana uende kwenye nyumba za watu bila shida ya maana ukijifanya kuwatembelea huku huna jipya mpaka mwenyeji wako anashindwa kufanya mambo yake kisa wewe hutoki je unataka mwenyeji akuage wewe aondoke ? au wewe umuage mwenyeji yeye uondoke?
Simu zipo, Posta zipo na mawasiliano mengine yapo. 'Kwanini Uende Ugenini Bila Taarifa' hata kwenda kijijini tuma taarifa ili mwenyeji ajiandae.
Aksanteni sana Tushirikiane Tafakari ya kesho
Umojamatukio Blog (UmB)
Toa Maoni , ushauri , Email , Charleslucas800@yahoo.com
Mobile. 0755851441 / 0718 138527
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment