KAURI YA LEO SEHEMU YA 2
‘KWANINI UOMBE KAZI KISHA UWANUNIE
UNAOWAHUDUMIA’ ?!’
‘Tutafakari pamoja’
Ndugu mpenzi
Mtazamaji na msomaji wa ukurasa huu au koramu hii ya Mtandao wa Umojamatukio
Blog (UmB) karibu kwa mara nyingine katika Tafakari ya Leo ikiwa ni sehemu ya
pili
ya mfurulizo wa
tafakari ya kila siku, leo tutajikita katika kero nyingine inayohusu jamii
inayotokana na wahudumu au baadhi ya watumishi katika sekta mbalimbali zikiwamo
sekta za Umma na binafsi. Karibu
Katika nchi yetu
limekuwa si jambo geni kukumbana na vituko unapokwenda katika ofisi au mahala
pa kupata huduma iwe ya kibiashara au huduma ya kijamii ikiwamo huduma za afya
na nyinginezo.
Baadhi ya
wahudumu katika maofisi utawakuta wakiwa hali ya kununa hata ukashindwa kuelewa
hali hiyo inatokana na tatizo gani ilhali wewe mhudumiwa ndiyo mara ya kwanza
kufika katika ofisi hiyo !
Kama hiyo
haitoshi utawakuta wakiwa katika mazungumzo yasiyokoma hata unapojaribu
kuwajulia hali huonekana kutokujali wala kustuka kuwa kuna mgeni na kibaya
zaidi ikihitaji msaada hutoa lugha ya ukali isiyo ya kiungwana kana kwamba
hawana jukumu ndani ya ofisi husika ‘Unaniangalia kwani mimi ndiyo
nilikusababishia huo ugonjwa si uliupata kwa kiherehere chako’ mfano moja ya
majibu katika baadhi ya hospitali za Umma, najiuliza tena kwanini Uombe kazi
tena muda mrefu wa kufuatia ajira hiyo kisha uje uwanunie unaowahudumia’.
Katika eneo
jingine hata ofisi binafsi kumeingia kero hii unafika kupata huduma ambayo
wameiombea leseni serikalini kwa ahadi kuwa watawahudumia wateja wao (wananchi)
kwa ukamirifu lakini kinachotokea ni usumbufu usiojali masharti ya leseni
inayoruhusu kufanya biashara au huduma husika,
Moja ya mifano ni
katika baadhi ya mabenki utakuta vidilisha vya huduma (Tillers) vikiwa zaidi ya
10 lakini cha ajabu ni vidisha viwili tu kama si kimoja kinachotoa huduma !!..
hapo unajiuliza hali hiyo inayosababisha msululu wa wateja ndani ya benki
husika una tija gani kwao ? unakosa jibu na kubwa zaidi utakuta wahudumu hao
wakionekana kuzunguka huku wakiwa hawajali usumbufu wanaosababisha, najiuliza
tena kwanini Uombe kazi kisha uwanunie na kuwasumbua unaowahudumia ? Tutafakali
pamoja.
Aksanteni sana subiri neno la kesho
Changia maoni,
charleslucas800@yahoo.com
0755 851441/ 0718
138527
No comments:
Post a Comment