Saturday, March 15, 2014

TUTAFAKARI PAMOJA






           KAURI YA LEO  SEHEMU YA 2
             
 ‘KWANINI UOMBE KAZI KISHA UWANUNIE UNAOWAHUDUMIA’ ?!’
               
                   ‘Tutafakari pamoja’



Ndugu mpenzi Mtazamaji na msomaji wa ukurasa huu au koramu hii ya Mtandao wa Umojamatukio Blog karibu kwa mara nyingine katika Tafakari ya Leo ikiwa ni sehemu ya pili 
ya mfurulizo wa tafakari ya kila siku, leo tutajikita katika kero nyingine inayohusu jamii inayotokana na wahudumu au baadhi ya watumishi katika sekta mbalimbali zikiwamo sekta za Umma na binafsi. Karibu

Katika nchi yetu limekuwa si jambo geni kukumbana na vituko unapokwenda katika ofisi au mahala pa kupata huduma iwe ya kibiashara au huduma ya kijamii ikiwamo huduma za afya na nyinginezo.

Baadhi ya wahudumu katika maofisi utawakuta wakiwa hali ya kununa hata ukashindwa kuelewa hali hiyo inatokana na tatizo gani ilhali wewe mhudumiwa ndiyo mara ya kwanza kufika katika ofisi hiyo !

Kama hiyo haitoshi utawakuta wakiwa katika mazungumzo yasiyokoma hata unapojaribu kuwajulia hali huonekana kutokujali wala kustuka kuwa kuna mgeni na kibaya zaidi ikihitaji msaada hutoa lugha ya ukali isiyo ya kiungwana kana kwamba hawana jukumu ndani ya ofisi husika ‘Unaniangalia kwani mimi ndiyo nilikusababishia huo ugonjwa si uliupata kwa kiherehere chako’ mfano moja ya majibu katika baadhi ya hospitali za Umma, najiuliza tena kwanini Uombe kazi tena muda mrefu wa kufuatia ajira hiyo, kisha uje uwanunie unaowahudumia’.

Katika eneo jingine hata ofisi binafsi kumeingia kero hii unafika kupata huduma ambayo wameiombea leseni serikalini kwa ahadi kuwa watawahudumia wateja wao (wananchi) kwa ukamirifu lakini kinachotokea ni usumbufu usiojali masharti ya leseni inayowaruhusu kufanya biashara au huduma husika.

Moja ya mifano ni katika baadhi ya mabenki utakuta vidirisha vya huduma (Tellers) vikiwa zaidi ya 10 lakini cha ajabu ni vidirisha viwili tu kama si kimoja kinachotoa huduma ajabu ?!!.. hapo unajiuliza hali hiyo inayosababisha msululu wa foleni ya wateja ndani ya benki husika una tija gani kwao ? unakosa jibu na kubwa zaidi utakuta wahudumu hao wakionekana kuzunguka huku wakiwa hawajali usumbufu wanaosababisha, najiuliza tena hata viongozi wao  'Kwanini Muombe kazi kisha muwanunie na kuwasumbua mnaowahudumia ? Tutafakali pamoja tujirekebishe.

             Aksanteni sana tusubiri neo la kesho

                  Changia maoni charleslucas800@yahoo.com  
                        0755 851441/ 0718 138527

No comments:

Post a Comment