Monday, April 14, 2014

BENKI ZA NMB NA DCB ZADHAMINI MAONESHO YA WANAWAKE WAJASILIAMALI

Ofisa Mikopo wa Benki ya NMB, Domitila Wapalila (kulia), akizungumza na wateja wapya wa benki hiyo waliofungua akaunti za 'Chap Chap', wakati wa maonesho ya Wanawake wajasiliamali Viwanja vya Mwembe Yanga Tandika.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB,  Joyce Kirasala, (wa pili kulia), akizungumza na mteja mpya  (kulia) aliyefungua akaunti ya ' Chap Chap'  wakati wa maonesho hayo
                                              
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Women And Youth Development Society, Sophia Mwakagenda (kulia), akizungumza na baadhi ya wanawake wajasiliamali wakati wa maonesho hayo. ya Siku 3

              Baadhi ya wanawake wakiwa katika banda la Benki ya NMB, wakifungua akaunti za ' Chap Chap'
               Wanawake wakiwa katika 'Mduara' wakicheza muziki katika maonesho hayo.
   Meneja Maendel;eo ya Bidhaa na Masoko wa Benki ya DCB Plc, Prochest Kachenje (katikati), akiwapa vipeperushi wateja waliofungua akaunti, wakati wa maonesho hayo.


              Baadhi ya wajasiliamali wanawake wakisoma vipeperushi vya Benki ya DCB Plc, wakati wa kabla ya kufungua akaunti katika banda la benki hiyo, wakati wa maonesho hayo. Benki hiyo imeshawakopesha wanawake mikopo inayofikia zaidi ya sh. bilioni 98, kwa manispaa zote za jiji la Dar es Salaam
Wanawake wajasiliamali kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya za Jiji la Dar es Salaam wakisikiliza maelezo kuhusu uwezeshaji katika ujasiliamali kutoka kwa mtoa mada (hayupo pichani), wakati wa maonesho hayo.

No comments:

Post a Comment