Tuesday, April 22, 2014
CHADEMA KARATU YAMSHUKURU RAIS KIKWETE
CHADEMA KARATU YAMSHUKURU RAIS KIKWETE
CHADEMA yamshukuru Rais Kikwete kwa maendeleo
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchangia
kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Wilaya ya Karatu katika Mkoa wa Arusha.
Aidha, chama hicho kimempongeza Rais Kikwete kwa kusambaza maendeleo kwa Watanzania wote bila kujali msimamo wao wa kisiasa na hata katika maeneo yanayounga mkono upinzani.
Shukurani na pongezi hizo zimetolewa mchana wa leo, Jumanne, Aprili 22, 2014 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Mheshimiwa Lazaro Titus Massey wakati wa sherehe za uzinduzi wa jengo la Halmashauri hiyo mjini Karatu. Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaongozwa na CHADEMA.
“Ni lazima tutoe shukurani nyingi kwako Mheshimiwa Rais kwa sababu bila wewe kuwa Rais wa Tanzania sisi Karatu tusingepata jengo hili. Pamoja na kwamba Halmashauri yetu ni CHADEMA bado umeamua kuchangia sana maendeleoya Wilaya yetu kwa kuchangia kiasi kikubwa ujenzi wa jengo hili. Sisi hata
ya fedha za ujenzi huu hatukuweza kuzitoa,” amesema Mheshimiwa Massey huko akishangiliwa na wananchi.
Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Karatu limegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.412 na kati ya hizo, Serikali imetoa shilingi bilioni 1.394 na Halmashauri imechangia shilingi milioni 18 tu.
Akizungumza baada ya kumsikiliza Mheshimiwa Massey, Rais Kikwete amesema kuwa ni sera ya Serikali yake kusambaza maendeleo kwa Watanzania wote bila kujali misimamo yao ya kisiasa wala kuongozwa na hisia nyingine mbali na ukweli kuwa kila Mtanzania anataka na anayo haki ya kupata maendeleo.
“Sisi hatuna wasiwasi, wananchi wa Karatu wamechagua CHADEMA lakini chama hiki hakina Serikali. Wananchi wamechagua chama bila Serikali. Halmashauri mnayo lakini Serikali tunayo sisi. Katika kusambaza maendeleo, sisi hatuwezi kubagua. Hiyo ndiyo demokrasia na Serikali yetu inaheshimu sana demokrasia na misingi ya utawala bora,” amesema Rais Kikwete.
Wakizungumza baadaye kwenye mkutano wa hadhara wabunge wote wawili wa
, waheshimiwa Cecilia Paleso na Israel Nanse wamerudia tena kumpogeza Rais Kikwete kwa kusambaza maendeleo katika maeneo yote ya Tanzania yakiwemo yaliyoko chini ya wapinzani.“Chini ya uongozi wako, maendeleo yamesambazwa na sisi Karatu tumenufaika sana. Ni matumaini yetu kuwa chini yako, tutaendelea kunufaika na sera
zako sahihi,”amesema Mheshimiwa Paleso.
Naye Mheshimiwa Nanse amesema: “Mheshimiwa Rais sisi kwetu hapa hatuna ugomvi kati ya vyama vya siasa. Siye CHADEMA tunajua kuwa CCM ni chama tawala Tanzania na CHADEMA ni chama kiongozi hapa kwetu Karatu. Ni uhusiano huu uliowezesha Karatu kuendelea kupata maendeleo.”
“Tunakushukuru na kukupongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kuifungua nchi yetu kwa barabara kila mahali. Aidha, sisi wana-Karatu tunakushukuru sana kwa
mradi wa maji ambao umeuzindua leo”. Tunakushukuru sana.
Rais Kikwete alikuwa katika ziara ya siku moja wilayani Karatu, Mkoa wa
Arusha na kesho atafanya ziara ya Wilaya ya Mwanga katika Mkoa wa Kilimanjaro.
VETA KUSHIRIKI MAONESHO YA WAJASILIAMALI WABUNIFU GABON
Na Charles Lucas
KIKUNDI cha wajasiliamali wabunifu wa biashara cha Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Ufundi Stadi (VETA) Chang'ombe Jijini Dar es Salaam cha Ngarawa, kimepata fursa ya kushiriki katika maonesho ya ujasiliamali na ubunifu wa biashara yatakayofanyika nchini Gabon Mwezi Desemba Mwaka huu.
Fursa hiyo wameipata baada ya kuwa washindi wa kwanza katika maonesho ya mwaka huu ya ITS TYME yaliyoandaliwa na Tassisi ya Utoaji Mafunzo kwa Wajasiliamali Vijana na Wanafunzi katika shule mbalimbali nchini ya Junior Achievement Tanzania (JAT) na kudhaminiwa na Benki ya Barclays Tanzania yaliyofanyika juzi jijini.
Pamoja na tiketi ya kushiriki maonesho hayo maku=mbwa ya nchi za Afrika pia VETA ilijinyakulia zawadi ya sh. 600,000 na cheti cha ushiriki ushindi huo imeupata baada ya kushiriki mara kadhaa ambapo ilishivinda vikundi 12 vilivyoingia fainali hiyo.
Vikundi vingine vilivyopata nafasi za juu na kujinyakulia sh. 300,000 kila kimoja vikundi hivyo ni Aslam na Lailat ambavyo mbali na fedha pia vilipata vyeti vya ushiriki wa mashindano hayo.
Akizungumza wakati wa fainali hizo Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Maria Ngowi alisema anawapongeza washiriki wote kwa mtu mmoja mmja au kikundi kwa moyo wa kujituma hadi kufikia hatuia hiyo ambayo itawajengea uwezo wa ubunifu katika kujiletea maendeleo.
Pia aliongeza kuwa zawadi zilizotolewa ni changamoto ya kuhamnasisha wala si kuonesha kuwa wale ambao hawakupata hawana uwezo ilia inafanyika hivyo ili kujenga hali ya kujituma kufikia malengo kwaashiriki na kuishukuru Benki ya Barclays Tanzxania kwa uamuzi wake wa kudhamini mashindano hayo kwa Mika 3 zaidi ambapo hatua hiyo itaongeza idadi ya wanafunzi na vijana kujitegemea wakiwa masomoni na baada ya kumaliza masomo.
Na Mkuu wa Mahusiano wa benki hiyo Neema Singo alisema benki hiyo itaendelea kudhamini shindano hilo baada ya kuona mafanikio katika kipindi cha mika iliyofanya udhamini huo na kuopongeza JAT kwa mafanikio yaliyofikiwa.
'Ni lengo la benki kuona kupitia udhamini huu Tanzania inaondokana na vijana tegemedhi wakiwa shule na baada ya kuhitimu kwani kupitia mpango huu kila kijana ataweza kujitegemea baada ya kupata mafunzo'
Na Mratibu wa Taasisi hiyo nchini Hamis Kasongo alisema mashindano hayo yalishafanyika katika nchi mbalimbali za Afrika zikiwamo Ghana, Zambia na Kenya ambapo JAT ilipeleka washiriki na kushinda vikombe mbalimbali kutokana na ubora wa bidhaa na ubunifu katika mchanganuo wa kibiashara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment