Tuesday, April 22, 2014
JUNIOR ACHIEVEMENT TANZANIA YAPATA WASHINDI SHINDANO LA ITS TYME 2014
Mratibu wa Taasisi ya Junior Achievement Tanzania (JAT), Hamis Kasongo akizungumza na waandishi wa habari wakati fainali za shindano hilo Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam yaliyodhaminiwa na Barclays Benki Tanzania.
Baadhi ya washiriki wa shindano la ubunifu wa wajasiliamali kibiashara wakisikiliza matokeo ya washindi wa shinandano hilo
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Maria Ngowi akizungumza na wajasiliamali washiriki wa shindano mara baada ya kutangazwa washindi Kampuni Garawa VETA ambao watakwenda nchini Gabon Mwezi Desemba
Mshindi wa Tatu wa Shindano hilo wa Kampuni ya Aslam akipokea kitita cha Sh. 300,000 kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Barclays Neema Singo (wa pili kulia). Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Maria Ngowi na Mratibu Hamis Kasongo
Mkurugenzi Mtendaji (kulia) akizungumza na baadhi ya washiriki kabla ya majaji kupita katika bidhaa mbalimbali
Mwakilishi wa washindi wa Kwanza wa shindano hilo kutoka VETA, Richard Mbanga (kushoto) akipokea kitita cha sh. 600,000 kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Barclays Benki Neema Singo (katikati) washindi hao watakwenda katika fainali za Afrika nchini Gabon Mwezi Desemba mwaka huu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment