Monday, June 30, 2014

KAMPUNI LA SIMU LA VIETTEL KUTOKA VIETNAM KUWEKEZA SEKTA YA MAWASILIANO VIJIJINI




Na Mwandishi  Maalumu

Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Juni 30, 2014, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka kampuni ya simu ya Viettel kutoka Vietnam ukiongozwa na  Le Dang Dung ambaye ni Makamu wa Rais wa Kundi la makampuni ya Viettel Group.

Kwenye mkutano huo uliofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, Le Dung amefuatana na Tao Duc Thang ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Shughuli za Kimataifa za Kampuni hiyo – Viettel Global.

 Dung amemwelezea Rais Kikwete kuhusu mipango ya Viettel kuwekeza katika shughuli ya mawasiliano ya simu hasa kwa maeneo ya vijijini.

No comments:

Post a Comment