Na Mwandishi Maalumu
Nchi
za Afrika zinatakiwa kuwa na msimamo mmoja kuhusu jinsi ya kukabiliana na
madhara ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa barani Afrika.
Misimamo
huo wa Afrika unatarajiwa kuwasilishwa kwenye mkutano mkubwa wa Dunia
kuhusu masuala ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa unaotarajiwa kufanyika New
York, Marekani Mwezi Septemba, 2014.
Akiwakilisha
ripoti ya Kamati ya Viongozi wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa
Duniani, tarehe 27 Juni,2014 katika Mkutano wa Viongozi wa Afrika (AU),
Rais Kikwete amesema kamati yake inataka kujikita na kujihusisha na
masuala yanayohusu fedha na teknolojia, hatua za kupunguza madhara,
na hatua mtambuka ambazo zitahusisha progamu za vijana, wanawake na hata
kuhusisha Balozi mbalimbali za Afrika katika suala zima la mabadiliko ya
hali ya hewa na pia kuhusisha Jumuiya ya Kimataifa na kufuatilia mapendekezo
mbalimbali.
Na Mwandishi Maalumu
Rais ameziasa Nchi za Afrika kuwa na utashi wa kisiasa na lengo la pamoja katika kukabiliana na suala hili ili kufanikisha lengo la dunia la hali ya hewa katika kipindi cha nusu ya pili ya karne ijayo.
Rais
amesema, ili kufanikisha juhudi mbalimbali, Bara la Afrika linahitaji msaada
mkubwa wa fedha na teknolojia ya kisasa.
Mapema
katika kikao cha Kamati ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa ambacho pia kimehudhuriwa
na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Bwawa Ban Ki Moon, Rais Kikwete amesema
mkutano ujao wa UN kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani ni chachu ya
makubaliano ya Mkataba wa Hali ya Hewa ifikapo 2015.
Ripoti
za karibuni kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa inaonesha kuwa hali ya Kilimo,
Afya, Maji na Nishati ziko hatarini na kwamba joto duniani limepanda kwa
sentigredi 0.85, hali ambayo inaashiria hali mbaya.
Mkutano wa Viongozi wa
Afrika (AU) umekamilika tarehe 27 jioni na Rais Kikwete anatarajiwa kurejea
nyumbani tarehe 28 Juni, 2014.
No comments:
Post a Comment