Na Mwandishi Maalumu
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa anakusudia kurejea darasani
kushika tena chaki kwa kuwa mhadhiri kwenye Chuo cha Taifa cha Ulinzi – National
Defence College (NDC) cha Dar Es Salaam.
Rais
Kikwete amelieleza hilo mchana wa leo, Ijumaa, Juni 20, 2014, wakati alipotoa Mhadhara
(Lecture)
kuhusu Usalama wa Taifa (The Security of the Nation) mbele
ya wanafunzi wa Chuo hicho kilichoko Kunduchi, Dar Es salaam.
Rais
Kikwete amewaambia wanafunzi wa kozi ya pili ya Chuo hicho kutoka nchini na
nchi za jirani za Uganda, Kenya na Rwanda: “Najisikia mwenye raha sana kuweza kurudi
darasani kutoa mhadhara huu. Tukio hili linanikumbusha enzi zangu katika Chuo
cha Kijeshi cha Monduli (TMA). Ni matarajio yangu pia kuwa nitaweza kurudi kuwa
mhadhiri katika Chuo hiki baada ya kukamilisha kazi yangu ya sasa.”
Rais
Kikwete ambaye alizungumza kwa kiasi cha saa mbili, alianza mhadhara wake baada
ya kupata maelezo kuhusu maendeleo ya Chuo hicho na baadaye akajibu maswali ya
wanafunzi ambao walimwuuliza kuhusu mambo mbali mbali yanayohusiana na usalama
wa nchi.
NDC
kilianzishwa rasmi Septemba 2, mwaka 2012 na Chuo hicho kilizinduliwa Rais na
Rais Kikwete Septemba 10, mwaka huo huo, 2012 wakati alipotembelea Chuo hicho
kwa mara ya kwanza kufuatia juhudi kubwa za uongozi wake kuhakikisha kuwa chuo
cha namna hiyo na cha aina yake kinaanzishwa nchini. Rais pia alifungua kozi ya
kwanza ya Chuo hicho.
Kundi
la wanafunzi wa kwanza kwenye Chuo hicho lilimaliza mafunzo yake Julai 23,
mwaka 2013 na sasa chuo hicho kinaendesha kozi ya pili yenye wanafunzi 30. Chuo
hicho tayari kimepata usajili kamili wa NECTA ambako kina uwezo wa kutoa
shahada ya uzamili katika masomo ya Strategic
Studies.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
IKULU
No comments:
Post a Comment