Thursday, June 26, 2014

HATUA MADHUBUTI ZICHUKULIWE KUZUIA MADHARA ZAIDI YA MABADIRIKO YA TABIA NCHI - KIKWETE




Na Maalumu

KUTOKANA na kiwango kilichofikiwa cha Tabia Nchi hivi sasa, nchi za  Afrika  hazina budi kuungana na kuchukua hatua za kupunguza madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa pamoja.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo tarehe 25 Juni,2014 Mjini Malabo, Equatorial Guinea wakati  akifungua Mkutano wa Wakuu wa Nchi 11 zinazounda Kamati  ya Mazingira ya Nchi za  Umoja wa Afrika au  Commitee of African Heads of States and Government on Climate Change (CAHOSCC).

"Suala la Tabia Nchi  baranil Afrika ni changamoto na fursa pia kwani kama tukifanya uamuzi mzuri tunaweza kupata manufaa kutokana na mbinu mbalimbali zilizopo  za kupunguza madhara yake".

Rais  Kikwete amesema na kuzitaka nchi kulichukulia suala la Tabia Nchi kwa umakini mkubwa kwani kwa hali tuliyofikia hivi sasa, hakuna chaguo lingine bali kuangalia njia za kupunguza athari zake tu.

Nchi wanachama wa Kamati ya Mazingira  ya AU in Tanzania ambaye ndiye Mwenyekiti, Algeria, Ethiopia, Congo-Brazaville, Kenya, Mauritania, Mauritius, Msumbiji na Uganda.

Kamati ya Mazingira ya AU ina jukumu la kuongoza nchi za Afrika katika kupanga mikakati, mbinu na njia mbalimbali za kukabiliana na madhara ya Tabia Nchi barani Agrola na pia kuzitumia changamot zake katika kuleta maendeleo na matokeo chanya  katika jitihada hizo kwa manufaa ya nchi za Afrika.


Kamati ya AU imesisistiza kuwa  nchi za Afrika zinahitaji kuboresha uwezo wake wa kupata taarifa za tahadhari katika ngazi zote, uwezo wa kifedha, mawasiliano na usafirishaji katika miji yake na pia kuongeza uwezo wake wa kuzuia mafuriko kwa kutumia njia za kisasa, uwezo wa kupanga miji na kupunguza athari za sasa na baadaye kwa ajili ya wananchi wake na  uchumi pia.

Amesema pia bara la Afrika linahitaji elimu na maarifa  zaidi kwa wananchi wake kwa ujumla kuhusu athari hizi na tahadhari kwa ujumla.

Rais amesema pamoja na  kwamba nchi za Afrika zinachangia asilimia ndogo katika suala la Tabia Nchi, Afrika haina budi kuzitaka nchi zinazoendelea kuchangia zaidi katika mahitaji na juhudi mbalimbali za  bara la Afrika katika jitihada zake za kupambana na athari za Tabia Nchi.

Rais Kikwete yuko Malabo kuhudhuria kikao cha siku mbili I cha Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU) kinachoanza tarehe 26 Juni 2014 na kumalizika tarehe 27 Juni,2014.

Ajenda ya kikao cha Mwaka huu ni Kilimo na Usalama wa Chakula barani Afrika

No comments:

Post a Comment