Taarifa Maalumu
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumatatu, Juni 23, 2014, amekutana na kufanya mazungumzo na tajiri mkubwa zaidi
barani Afrika, Mfanyabiashara Aliko Dangote wa Nigeria.
Katika
mkutano huo uliofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, Bwana Dangote amemweleza Rais
Kikwete kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha saruji ambacho kinajengwa na
kampuni ya Bwana Dangote mjini Mtwara.
Bwana
Dangote amemweleza Rais Kikwete kuwa kiwanda hicho cha Mtwara kitakuwa kikubwa
zaidi kuliko kiwanda chochote cha saruji katika ukanda wa Afrika mashariki,
kati na kusini isipokuwa kile kinachojengwa Afrika Kusini.
Rais
Kikwete amekuwa anaweka msukumo wa kipekee katika ujenzi wa kiwanda hicho kwa
nia ya kuongeza uwekezaji nchini na pia kuinua kiwango cha saruji nchini.
Katika
jitihada zake hizo, Rais Kikwete mwezi uliopita alifanya ziara katika kiwanda
kikubwa zaidi kuliko vyote vya saruji katika Afrika kinachomilikiwa na Bwana
Dangote nchini Nigeria.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
No comments:
Post a Comment