Na Mwandishi Maalumu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumapili, Juni 22, 2014, amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Anne Wu
Suk Ching, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama Tawala cha Jamhuri ya Watu wa
China.
Katika
mazungumzo hayo, Rais Kikwete na Mheshimiwa Anne Ching wamejadili hali ya
uhusiano kati ya Tanzania na China na jinsi nchi hizo mbili zinavyoweza
kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo ulioanzishwa miaka 50 iliyopita.
Dkt.
Anne Ching pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Vituo vya Biashara Duniani, Tawi la
Hong Kong (World Trade Centre Association
Honk Kong) na pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Biashara ya China na Afrika,
Tawi la Hong Kong (China-Africa Business
Coundil Hong Kong Chapter).
Rais
Kikwete pia amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Mfalme Qaboos Bin Said wa Oman
uliowasilishwa na mjumbe maalum wa kiongozi huyo, Mheshimiwa Masoud Mohamed
Al-Ruqaishi, ambaye pia ni Balozi wa Oman katika Tanzania.
Baada
ya kupokea ujumbe huo, Rais Kikwete amemwomba Balozi huyo kuwasilisha shukurani
zake kwa Mfalme Qaboos kwa ujumbe huo maalum.
No comments:
Post a Comment