Monday, March 17, 2014
'KWANINI UMNUNIE ULIYEMPA LIFTI ? '
KAURI YA LEO
‘KWANINI UMNUNIE ULIYEMPA LIFT ?’, Tutafakari pamoja
Ndugu wapenzi wasomaji na watazamaji wa koramu hii ya Umojamatukio Blog (UmB) ninayofuraha kubwa kuwakaribisha katika tafakari ya leo ili tushiriki pamoja kujitathmini ‘ Kwanini Umnunie uliyempa lift ya gari lako ?’, karibuni.
Watanzania tunao utamaduni wa kiusaidiana katika mazingira yo yote bila kujali unayemsaidia ni ndugu, rafiki au mtu usiyemfahamu lengo likiwa ni kumpunguzia au kumuondolea shida aliyonayo kwa wakati huo au wakati ujao.
Lakini msaada kwa kawaida ili uwe na maana lazima umuachie heshima, uhuru, utu na furaha, anayesaidiwa vingine kama hautakuwa na maudhui hayo ni wazi utakuwa si msaada bali kero na utumwa wa kiana.
Katika jiji la Dar es Salaam usafiri ni jambo linalogonga vichwa vya wakazi wa jiji hilo kila uchao kutokana na jiografia ya miundombinu isiyotosheleza mahitaji ya wakazi wanaofikia milioni 5.
Katika hali hiyo usafiri ni suala tete na baadhi ya watu wenye usafiri binafsi hujitoa kuwasaidia wale wasio na magari hata pikipiki hilo ni jambo zuri.
Lakini katika hali ya kushangaza baadhi yao hutoa msaada wakiwa katika hali ya kujiamini au kutoikuwa na utayari hali ambayo husababisha kutokuwa na amani baada ya kutoa msaada huo wa lift.
Utakuta mtu katoa msaada mwenyewe kwa hiari yake lakini ukishaingia ndani ya gari uso hukunjamana mithili ya mtu anayetafuna ndimu hali ambayo humuweka katika mazingira magumu aliyesaidiwa, kama hiyo haitoshi mtu huyo akiingia kituo cha mafuta kujaza mafuta huanza kulalamika Oo!! Mafuta ghali hili gari nitaliacha nyumbani siwezi kuumia hivi! Hapo unajiuliza maneno hayo anaambiwa nani ?, Utajiuliza maneno hayo anaambiwa nai mwenye kituo au wewe uliyepata lifti? Sasa tutafakari wote Kwanini Umnunie Uliyempa Lifti ?.
Sasa unajiuliza ni nani alimnunulia gari /? Je hakujua kama gari hilo linatumia mafuta, lakini kikubwa zaidi tujiulize uliposimama na kumpa msaada huyo msaidiwa nani alifunga break ya gari ? kwanini hukupitiliza ikiwa hukupenda kumsaidia ?.
Kwa leo tuishie hapo lakini tutafakari tujirekebishe.
Tutafakari pamoja
Kwa maoni na Ushauri – charleslucas800@yahoo.com
0755 851441 / 0718138527
TAARIFA
Kutokana na hali isiyazuirika koramu hii itakuwa hewani kwa wiki mara tatu. Jumatatu, Jumatano na Jumamosi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment