Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa (kulia) akiwa na bibi yake, Consolata Semgovano wakipungia mikono wananchi, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kijiji alichozaliwa cha Magunga, Iringa Vijijini. Picha na Kamanda wa Matukio Blog.
Mkuu wa wilaya ya Makete, mkoani Iringa, Josephine Matiro (kushoto) akimkabidhi sehemu nya msaada wa bati, Ami Mahenge ambaye ni mmoja kati ya waathirika wa kimbunga katika Kijiji cha Ndulamo wilayani humo hivi karibuni. Picha na Michuzi Blog.
Baadhi ya wakazi wa Ilala, Sharif Shamba wakifukia dimbwi la maji katika barabara ya mtaa huo, kama walivyokutwa Dar es Salaam jana. Barabara hiyo haipitiki kutokana na kuwapo kwa vifusi ambavyo havijasambazwa.
MAANDAMANO SHOPRITE
Baadhi ya wafanyakazi wa maduka mbalimbali ya Kampuni ya Shoprite Chekers Limited. wakiwa katika viwanja katika ofisi za Chama cha Wafanyakazi TWICO Kanda ya Ilala ili kudai haki yao ya matibabu na malipo ya likizo. Pia walisema wanahofia maduka hayo kuuzwa kwa mwekezaji mwingine kabla ya kulipwa stahili zao
No comments:
Post a Comment