Walemavu wanaojishughulisha kuomba misaada kwa wasamaria katika makutano ya Barabara za Azikiwe na Bibi Titi Mohamed, wakihudumiwa na mchuuzi wa matunda (katikati), kanma walivyokutwa Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kushoto) akibonyeza kitufe cha kompyuta ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi huduma mpya kwa wateja ya 'NBC Direct', Dar es Salaam jana. Wengine ni baadhi ya maofisa wa benki hiyo, Sarah Laiser-Sumaye, Mary Kapeja, Andrew Massawe na Mussa Jallow ambaye ni Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki hiyo.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime (kushoto), akiteta na washitakiwa wengine, wakati wa kutajwa kwa kesi ya mauaji ya kukusudia inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam juzi. kesi hiyo inahusu jengo la ghorofa lililoporomoka na kuua watu 27 katika Mtaa wa Indira Ghadhi.
Doris Malulu wa TBL akitoa zawadi kwa baadhi ya wadau wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), walipotembelea kiwanda cha Dar es Salaam juzi ili kuona uzarishaji wa bia unavyofanyika.
Baadhi ya waendesha pikipiki za gurudumu tatu Bajaj wenye ulemavu wakijadiliana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam jana, walipopeleka malalamiko ya kuzuiwa kubeba abiria katikati ya jiji.
No comments:
Post a Comment