Sunday, March 16, 2014



                                     WATEJA WAZAWADIWA BIDHAA ZA SAMSUNG

Kampuni ya Samsung Tanzania imeendelea kuwaneemesha wateja kwa kuwazawadia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na kampuni hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi zawadi mbalimbali kwa wateja Dar es Salaam jana, Mwakilishi wa kampuni hiyo nchini Ibrahim Kombo, alisema Samsunga Tanzania imejipanga kuhakikisha wateja wanafurahia huduma zao.

Katika kudhihirisha hilo kampuni hiyo itaendelea kutoa zawadi kwa kila mteja atakayenunua bidhaa zao halisi na kuongeza kuwa kila bidhaa itakayouzwa itapata dhamana ya Miaka 2 ili kumhakikishia mteja usalama na thamani ya fedha yake.

Kombo aliongeza kuwa promosheni hiyo itafanyika kila mwisho wa mwezi bila kikomo na kuwataka watanzania kushiriki kununua bidhaa za aina zote za kampuni hiyo.

Jumla ya wateja wanne walikabidhiwa zawadi zao zikiwamo simu, luninga, jimbo na vifaa vya muziki na wateja wenguine watakadhiwa zawadi zao kupitia matawi yaliyopo mikoani.

Waliochukua zawadi zao ni wakazi wa jijini, Faril Sheral, Joseph Nswila, John Macharia na Lugano Msokwa.

No comments:

Post a Comment