Na Anna
Titus
Kukosekana kwa ofisi ya Serikali za
Mitaa Igunga Kunashusha Hadhi ya Kuwa Wilaya
“Ni aibu kwa
Wilaya yenye zaidi ya miaka 40 kukosa ofisi za Serikali ya Mtaa”
KATIBA ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inafafanua
kuwa Serikali za mitaa ni vyombo vya wananchi vilivyopo katika ngazi ya msingi ya
serikali.Serikali za Mitaa huundwa,huendeshwa,husimamiwa na kuwajibika kwa
wananchi wenyewe. Hivyo basi Serikali za mitaa zimeundwa kwa mantiki ya
kuwawezesha Wananchi, wanaume kwa wanawake,kushiriki katika masuala ya
siasa,uchumi,upatikanaji wa huduma na utawala katika maeneo yao na katika nchi
yao.Kwa ujumla ni muundo ambao unawawezesha wananchi kuwa na udhibiti wa
maamuzi ya wawakilishi waliowachagua. Kwa mtazamo huu wa kikatiba,serikali za
mitaani fursa kwa wanajamii kukuza demokrasia na ushiriki wao katika maendeleo
ya maeneo yao.Ni vyema ieleweke kuwa serikali za mitaa si wakala wa serikali
kuu bali ni Serikali kamili zenye mamlaka chini ya sheria.Kwa mujibu wa Katiba
ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania,Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote na
serikali inapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi.Hii ndiyo
maana hasa ya kupeleka madarakakwa wananchi.
Kuundwa kwa
vitongoji ni mojawapo ya marekebisho yaliyofanywa siku za karibuni ili kuboresha
muundo wa serikali za Mitaa.Lengo la serikali la kuanzisha vitongoji ni pamoja
na kuimarisha demokrasia kwa wananchi,na kuziba pengo lililoachwa baada ya
kuondolewa wajumbe wa Nyumba kumikumi waliokuwa chini ya mfumo wa chama kimoja
cha kisiasa.Kuwepo kwa vitongoji kunatoa fursa kwa wananchi kushiriki kimoja
katika siasa ya vyama vyingi kwa ngazi ya msingi kabisa.Ni jambo la kawaida
kukuta kuwa wenye viti wa vitongoji mbalimbali katika kijiji kimoja wanatoka
kwenye vyama tofauti vya siasa.
Katika hali
ya kushangaza Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora ni moja kati ya Wilaya kubwa
katika mkoa huo lakini cha kushangaza ni kukosekana kwa ofisi ya serikali za
mitaa kama ilivyo sehemu nyingine.
Abdalah Said
ni mwenyekiti wa mtaa wa Stoo ya Pamba anasema,wilaya hiyo ilianzishwa Mwaka
1975 na mwaka 1976 ndipo ulifanyika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa.
Lakini mpaka hivi leo katika wilaya hiyo hakuna kitu kinachoitwa ofisi ya
Serikali za mitaa.
“sisi
wenyeviti tunashindwa kufanya kazi kwa kuweka kumbukumbu za taarifa za wananchi
kwa usahihi kutokana na kukosekana kwa ofisi hizo,shughuli zote tunafanyia
majumbani kwenu yani katika makazi tunayoishi na familia zetu ndipo ofisi
zilipo,hivyo kwa kukosa ofisi ya kuendeshea shughuli inapelekea sisi kukosa
kumbukumbu stahiki na sahihi zinazoonyesha uhalali wa wanannchi”anasema.
Aliongeza
kuwa vifaa vyote vya ofisi vinakaa nyumbani kitu ambacho si salama na hakileti
tija ya uongozi kwani kazi za ofisini ni tofauti na kazi za nyumbani na ndio
maana maofisi yote hukaa mbali na nyumbani kwa ajili ya kuepusha adha na
usumbufu mbalimbali ambao kwa namna moja ama nyingine yaweza kuwa ni tatizo.
Aidha
Mwenyekiti huyo alisema, “tangu mwaka 2010 tuliahidiwa kuanzishwa kwa mji mdogo
na ofisi zitajengwa lakini tangu mwaka huo hakuna kinachoendelea,tumekuwa watu
wa kupewa ahadi hewa kila kukicha hata karatasi kwa ajili ya shughuli za
kiofisi tumekuwa tukijinunulia wenyewe. Mfano wagonjwa wenye msamaha hatuna
karatasi maalumu kwa ajili ya kuwapa kwenda kutibiwa zaidi ya kuchana katika
daftari na kumwandikia je kumbukumbu ziko yapi?”
Alisema
kuwa,wao kama wenyeviti wanafanya kazi katika mazingira magumu na hawana msaada
wowote,ila kappa wakipata ofisi ufanisi wao wa kazi utaongezeka zaidi.
Wakati
naendelea kufanya mazungumzo na mwenyekiti huyo nilishuhudia mwanamke mmoja
ambaye mwanae aligongwa na gari hivyo alikuja kwa ajili ya kuulizia kesi yake
inaendeleaje.
Kwa upande
wake mmoja wa wakazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Masanja
alisema,hiyo kama wilaya haistahili kuwa hivyo ilivyo na badala yake serikali
inatakiwa iboreshe kwani maendeleo yanaanzia chini.ofisi ya serikali za mitaa
ina maana kubwa sana kwani ndio mahala pekee ambapo unaweza kupata kumbukumbu
za wakazi wa eneo husika.
“unajua kama
kungekuwa hakuna umuhimu wa ofisi nadhani hakuna mtu yeyote ambaye angetoka
asubuhi na kwenda katika ofisi flani sisi wananchi tunapata shida sana kutokana
na kuwa mimi nimepata tatizo lakini tatizo langu sitaki mtu mwingine ajue zaidi
ya kiongozi wangu lakini ninapokwenda kwa mwenyekiti nakuta na familia yake ipo
nawezaje kuzungumza waziwazi huku familia yake ikinisikiliza? Ifike mahali
serikali itambue umuhimu wa hawa viongozi wa chini kwani bila hawa wao bado
hawajawa viongozi wan chi nzima ifikie kipindi watambue mchango wao ni upi
katika jamii”anasema Bw.Masanja
Naye
Bi.Ashura Ramadhan alisema wao wamekwisha zoea hali hiyo na wanaona ni kawaida
tu kwenda kwa mwenyekiti na kuelezea matatizo yako japokuwa si vyema lakini hii
inatokana na utendaji mbovu hasa wa mbunge wa jimbo hilo lenye zaidi ya miaka
40
“sisi kama
wananchi hali hii inakera sana kiukweli kwa sababu mimi si mzaliwa wa hapa huko
nilikotoka mambo kama haya hayakuwepo kama ukipata shida ya kwenda kwa
Mwenyekiti ni lazima utaenda katika ofisi yake na si nyumbani,ikitokea
umekwenda nyumbani ujue hiyo ni dharura au muda wa kazi umekwisha hivyo
itakulazimu uende nyumbani kwakwe. Lakini huku nyumba ya mwenyekiti ndio ofisi
ya Serikali ya Mtaa hadhi na heshima ya ofisi iko yapi?”alisema.
Majukumu ya Serikali za Mitaa
yanaangukia katika sehemu kuu nne ambazo kuwezesha na kudumisha utulivu, amani
na utawala bora, Kudumisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii na
miundo mbinu,Kuchochea maendeleo ya kiuchhummi na kijamii na Kulinda mazingira
kwa lengo la la kuchangia katika maendeleo endelevu.Utekelezaji wa majukumu haya unategemea jinsi ambavyo ngazi mbalimbali katika serikali za mitaa zinavyotekeleza wajibu na majukumu katika mfumo wote wa serikali za mitaa ili kuongeza ufahamu miongoni mwa wananchi.
Pamoja na kuwepo kwa
majukumu ya serikali za mitaa haya pia ni majukumu ambayo wananchi wanatarajiwa
kuyatekeleza, Kisheria na kiutawala wananchi
wanatarajiwa kutekeleza majukumu yafuatayo:kuelewa Sheria zote zinazohusu
serikali za Mitaa na kuishi kufuatana na sheria hizo,Kutambua nafasi yake
katika jamii na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo, Kudai haki
zake za msingi kutoka kwa viongozi wake,kuhakikisha kuwa viongozi wanatimiza
wajibu wao kama ipasavyo.
KITUO CHA HALI YA HEWA
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la ICIPE-CHIESA kutoka nchini Kenya, Dkt. Tino Johnson (wa pili kushoto), akikabidhi mtambo wa kituo cha hali ya hewa kilichojengwa kwa msaada wa Serikali ya Finland kwa ajili ya Mamlaka ya Hali ya Hewa, mkoani Kilimanjaro. Kulia ni mmoja wa wadau, Ruben Mashingia Kirua Vunjo Magharibi na Mtalaamu wa mambo ya maji wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa David Mwakalila. (Na Mpigapicha Wetu)
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda akiwaongoza madiwani wa manispaa hiyo wakati wa maziko ya Diwani wa Mbweni Bw.Boniface Nyachibwe yaliyokuwa mwishoni mwa wiki. Picha Charles Lucas
Mkazi wa Mbagala akchagua mafungu ya Zabibu zilizopangwa chini bila kujali afya yake katika barabara ya Kilwa,Mbagala kama alivyokutwa Dar es Salaam jana
Baadhi ya magari yakiwa yameegeshwa nje ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Azania Front Posta jana, Dar es Salaam kutokana na tatizo la maaegesho. (Picha na Charles Lucas
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bw. Tom Borghols (kushoto), akipeana mkono na Mkurugenzi wa Kampuni ya MIC Tanzania Limited 'TIGO', Bw. Ruan Swanepoel, mara baada ya kutiliana saini mkataba, Dar es Salaam hivi karibuni ambapo wateja watapata huduma za uhamishaji kifedha katika taasisi hizo. Kushoto ni Mkuu wa Kutengo cha Wateja Huduma Binafsi, Abdul Nsekela. (Picha na Charles Lucas)
Baadhi ya wakazi na watoto wa Jiji la Dar es Salaam, wakiwa katika matembezi ya hiari ya Kilometa 9, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani yaliyolenga kuongeza ufahamu kwa jamii kuhusu dalili za awali za Saratani ya watoto, yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Tumaini la Maisha Tanzania (TMT) kwa Kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Dkt. Marina Njelekela na Katikati ni Mkurugenzi wa shirika hilo. Janet Mbuguni. (Picha na Charles Lucas

No comments:
Post a Comment