Wednesday, February 26, 2014

YALIYOTOKEA LEO

MAPENDEKEZO YA ALAT KATIBA MPYA
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT), ambaye pia ni Meya wa Jiji  la Dar es Salaam, Mstahiki Dkt. Didas Masaburi, akionesha Katiba ya sasa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam jana, wakati akielezea nia ya jumuiya hiyo kufika bungeni ili kuwaomba wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba Mpya kuzungumzia na kutambua shughuli za jumuiya hiyo kikatiba. Kulia ni Ofisa Uhusiano na Habari wa jumuiya hiyo. Seif Hassan.

DHAMANA YA UWEKEZAJI
Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), Daudi Mbaga , akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam jana, kuhusu ongezeko la shughuli mbalimbali za uwekezaji na faida iliyopatikana nchini. Kushoto ni Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa mfuko huo, Simon Migangala.


Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Adam Malima akizungumza kartima Mkutano Mkuu wa PSPF, Dar es Salaam jana

MKUTANO MKUU PSPF
Baadhi ya wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wakimsikiliza mgeni rasmi Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka, Dar es Sa Salaam jana.

No comments:

Post a Comment