KAURI YA LEO SEHEMU YA 2
‘KWANINI UOMBE KAZI KISHA UWANUNIE
UNAOWAHUDUMIA’ ?!’
‘Tutafakari pamoja’
Ndugu mpenzi
Mtazamaji na msomaji wa ukurasa huu au koramu hii ya Mtandao wa Umojamatukio
Blog karibu kwa mara nyingine katika Tafakari ya Leo ikiwa ni sehemu ya
pili
ya mfurulizo wa
tafakari ya kila siku, leo tutajikita katika kero nyingine inayohusu jamii
inayotokana na wahudumu au baadhi ya watumishi katika sekta mbalimbali zikiwamo
sekta za Umma na binafsi. Karibu
Katika nchi yetu
limekuwa si jambo geni kukumbana na vituko unapokwenda katika ofisi au mahala
pa kupata huduma iwe ya kibiashara au huduma ya kijamii ikiwamo huduma za afya
na nyinginezo.
Baadhi ya
wahudumu katika maofisi utawakuta wakiwa hali ya kununa hata ukashindwa kuelewa
hali hiyo inatokana na tatizo gani ilhali wewe mhudumiwa ndiyo mara ya kwanza
kufika katika ofisi hiyo !
Kama hiyo
haitoshi utawakuta wakiwa katika mazungumzo yasiyokoma hata unapojaribu
kuwajulia hali huonekana kutokujali wala kustuka kuwa kuna mgeni na kibaya
zaidi ikihitaji msaada hutoa lugha ya ukali isiyo ya kiungwana kana kwamba
hawana jukumu ndani ya ofisi husika ‘Unaniangalia kwani mimi ndiyo
nilikusababishia huo ugonjwa si uliupata kwa kiherehere chako’ mfano moja ya
majibu katika baadhi ya hospitali za Umma, najiuliza tena kwanini Uombe kazi
tena muda mrefu wa kufuatia ajira hiyo kisha uje uwanunie unaowahudumia’.
Katika eneo
jingine hata ofisi binafsi kumeingia kero hii unafika kupata huduma ambayo
wameiombea leseni serikalini kwa ahadi kuwa watawahudumia wateja wao (wananchi)
kwa ukamirifu lakini kinachotokea ni usumbufu usio jali masharti ya leseni
inayoruhusu kufanya biashara au huduma husika,
Moja ya mifano ni
katika baadhi ya mabenki utakuta vidilisha vya huduma (Tillers) vikiwa zaidi ya
10 lakini cha ajabu ni vidisha viwili tu kama si kimoja kinachotoa huduma !!..
hapo unajiuliza hali hiyo inayosababisha msululu wa wateja ndani ya benki
husika una tija gani kwao ? unakosa jibu na kubwa zaidi utakuta wahudumu hao
wakionekana kuzunguka huku wakiwa hawajali usumbufu wanaosababisha, najiuliza
tena kwanini Uombe kazi kasha uwanunie na kuwasumbua unaowahudumia ? Tutafakali
pamoja
Aksanteni sana subiri neo la kesho
Changia maoni
charleslucas800@yahoo.com
0755 851441/ 0718
138527
KAURI YA LEO SEHEMU YA 1
‘Tutafakari pamoja’
‘Kwanini Uende
Bar ikiwa huna fedha’ ?
Ndugu wapenzi na
watazamaji na wasomaji wa Mtandao wa
Umojamatukio nikiwa founder wa mtandao huu nimetafakari nikaona kuna umuhimu wa
kuwapo kwa koramu itakayosaidia kurekebisha tabia zetu kwa msaada wa pamoja
kama jamii lengo kuu likiwa ni Kuburudisha Kuelimisha na Kutahadharisha kwa
manufaa ya jamii yetu.
‘Kwa leo tunaanza
kwa tafakari hii katikati head line hapo juu.’ Kwanini uende bar au katika
stare ilhali huna fedha’, karibuni
tuendelee
Kumemekuwapo na
baadhi ya watu wenye tabia inayoelekea kuchosha na kusumbua wengine hivi karibuni nikiwa katika mizunguko
mbalimbali ya kimaisha nilikumbana na kituko cha mtu aliyeonekana kama ni mtu
mstaarabu lakini cha ajabu aliingia katika Bar huko Mbagala na kuketi kwenye
kona kana kwamba anamsubiri mtu huku akiwa na chupa ya maji yaliyokuwa
yakikaribia kumalizika.
Lakini jambo la
ajabu mtu Yule alikuwa akiangazamithili ya mtu anayemsaka mbaya wake la hasha !
kumbe alikmuwa akitafuta mfadhili wa kinywaji lo ?! kilichonishangaza ni
ujasili wa mtu Yule kuomba pombe katika mazingira yale ambayo kwa kawaida kila anayekaribia huwa amejipanga kwa bajeti
yake.
Na kibaya zaidi
nilichokiona kwanini? ikiwa hana fedha awahi mapema bar kabla wenye nazo
hawajafika
katika hali ya
kawaida ni fedheha kuomba pombe kwani si kitu cha kipaumbele kwa kuishi kama
kilivyo chakula watu hawa hunoa ndimi za kinafiki kwa kujifanya wakiwasifu kwa
maneno ya ghiriba wenye nazo ili waonewe huruma hiyo ni aibu.
Kundi la watu wa
aina hii ni wengi wengine ni jirani zako wengine ni ndugu zetu basi naomba
tutafakari kwa makini kauri yetu ya leo kisha tuchukue hatua ya tujirekebishe
kwanini tuwasumbue wenye nazo ilhali hawakutuita kwenda kwenye starehe.
Aksanteni sana subiri neon
la kesho
Changia maoni
charleslucas800@yahoo.com
0755 851441/ o718
138527
No comments:
Post a Comment