Ofisa Mawasiliano
wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCCL), Mtanga Noor (kulia) akisalimiana na Mbunge
wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani 'Profesa Majimarefu' wakati wa hafla
ambapo kampuni hiyo ilikabidhi msaada wa mifuko 1000 ya saruji yenye thamani ya
sh. milioni 13.1 kujengea vyumba vya maabara katika shule za sekondari Wilayani
Korogwe. Katikati ni Mkuu wa wilaya hiyo, Mrisho Gambo. Hafla hiyo ilifanyika
Mjini Tanga juzi.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kufungua semina ya uwezekezaji ya Benki ya CRDB, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dkt. Charles Kimei.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Elias Kwesi (mwenye suti wa pili kushoto), akiongozana kwenda eneo la kuzindua rasmi mradi wa maji katika Zahanati ya Mvuti, Kata ya Msongola, Wilayani Ilala, Dar es Salaam jana, mradi uliojengwa na Kampuni Bia Tanzania (TBL). Wa pili kulia ni Mkuu wa mahusiano na sheria wa Kampuni hiyo, Bw. Stephen Kilindo, Diwani wa Kata hiyo, Angelina Malembeka na Ofisa Mauzo wa TBL Ilala, Bw. Godrack Kalebi
No comments:
Post a Comment