Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Perseko Kone kufuatia vifo vya watu 19 wakiwemo Askari Polisi wanne (4) na Viongozi watatu wa Kijiji kufuatia ajali ya barabarani iliyosababishwa na basi lililokuwa likitokea Kigoma kuelekea Dar es Salaam katika Barabara kuu ya Singida - Dodoma.
Ajali hiyo ilitokea
usiku wa tarehe 27 Aprili, 2014 katika Kijiji cha Utaho, Wilaya ya Ikungi
Mkoani Singida baada ya basi la Kampuni ya Sumry lenye Nambari ya Usajili T.
799 BTE aina ya Nissan kuwagonga watu waliokuwa wamekusanyika katika eneo
ambapo ajali nyingine ilikuwa imetokea wakiwa pamoja na Askari Polisi kutoa
msaada katika ajali nyingine iliyokuwa imetokea katika eneo hilo ambapo mwendesha
baiskeli aligongwa na lori na kufariki papo hapo.
“Nimepokea kwa
masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watu 19 wakiwemo Askari Polisi wanne na
Viongozi watatu wa Kijiji cha Utaho katika Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida. Vifo hivi vimetupotezea kama Taifa nguvu kazi
muhimu kwa ujenzi wa nchi yetu na hakika vimeacha simanzi na huzuni kubwa kwa
familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu”, amesema Rais
Kikwete katika Salamu zake.
Rais Kikwete
amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Perseko Kone kumfikishia Salamu
zake za Rambirambi na pole nyingi kwa watu wote waliopotelewa na ndugu na jamaa
zao kutokana na ajali hiyo, na amewahakikishia wafiwa kuwa yuko pamoja nao
katika kuomboleza msiba huo mkubwa.
“Ninamuomba
Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema awawezeshe kupona haraka na kurejea katika
hali zao za kawaida watu wote waliojeruhiwa katika ajali hiyo ili waweze kupona
haraka na kuungana tena na ndugu
No comments:
Post a Comment