Tuesday, April 29, 2014

MATUKIO MBALIMBALI JIJINI DAR ES SALAAM NA ZIARA AGA KHAN HOSPITALI YA WAKE ZA VIONGOZI WA KITAIFA

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Home Expo, Zenno Ngowi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam , kuhusu maonesho ya wadau wa nyumba na makazi yanayotarajiwa kufanyika Mwezi August Mwaka huu. Kushoto ni Meneja Masoko Oscar Mpenjuna na Meneja Biashara, Mathew Gugai.

Mke wa Makama wa Rais Aisha Bilal na Mke wa Waziri Mkuu Tunu Pinda (kulia), wakisikiliza maelezo kutoka kwa wataalamu wa ugonjwa wa saratani, Dkt. Amyn Alidina na Sulaiman Shahabudin  (kushoto) kuhusu tiba ya saratani mbalimbali ikiwamo  ya shingo ya kizazi kwa akinamama inavyotolewa katika Hospitali ya Aga Khan, wakati wa ziara ya kutembelea hospitali hiyo, Dar es Salaam  wiki hii


Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Flaviana Charles (katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam, kuhusu tamko la kuitaka Serikali kudhibiti baadhi ya taasisi zinazokopesha fedha kwa riba kubwa kitendo kinachosababisha baadhi yao kutapeliwa kwa dhamana ya ardhi na mali nyingine. Kushoto ni Meneja Miradi Husein Sengu na Wakazi wa Mkoa wa Arusha Bakari Mohamed Mji Mdogo Usariver na Rehema Salim kutoka Kata ya Akeri
Mke wa Makamu wa Rais Aisha Bilal akisalimiana na baadhi yta watendaji wa Hospitali ya Aga Khan wakati akiwasili na na msafara wa wake za viongozi mbalimbali kutembelea hospitali hiyo.

No comments:

Post a Comment