Thursday, April 3, 2014

MATUKIO MBALIMBALI YA JIJI LA DAR

   Gari likipita kando ya mkokoteni wenye ndizi eneo la makutano ya Barabara ya Uhuru na Nyamwezi, biashara hizo zimepigwa marufuku Katikati ya Jiji la Dar es Salaam.


  Mwakilishi wa Kampuni ya Samsung akikabidhi zawadi kwa mteja (kushoto), aliyeshinda jiko  baada ya kununua bidhaa za kampuni hiyo.

   Mkazi wa jiji jina halikufahamika akisafiri kwa gari lililobeba tofali kitendo kinachoweza kuhatarisha maisha yake, kama alivyokutwa makutano ya Barabara za Morogoro na Kawawa Magomeni, Dar es Salaam


          Mwakilishi wa Kampuni ya Samsung akikabidhi zawadi kwa mteja (kushoto), aliyeshinda jiko  baada ya kununua bidhaa za kampuni hiyo.
Askari wakimuandikia adhabu ya faini baada ya daladala hilo kukiuka taratibu za usafirishaji, kama walivyokutwa Barabara ya Uhuru Kariakoo , Dar es Salaam

Askari wa doria akiwazuia baadhi ya wakazi wa Mbagala Misheni, wasichukue mafuta ya kula baada ya gari lenye kontena kupinduka katika eneo hilo, Barabara  ya Kilwa.

Mwandishi na Mpigapicha wa gazeti ka Majira, Anna Titus(Kushoto) akipokea tuzo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mwananchi Communication Limited na Mkurugenzi wa Kazi Service Limited Bi.Zuhura Muro,wakati wa utoaji tuzo za uandishi wa habari zinazoandaliwa na EJAT zilizofanyika Mwaka 2013 Dar es salaam.

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Home Shopping Centra (HSC), Nathir Bahayan akimkabidhii Rehana Jaffer hundi ya sh.500,000 , baada ya kushinda zawadi hiyo katika mashindano yaliyokuwa yakiendeshwa na kampuni hiyo katika mtandao wa kijamii ambapo yeye aliweza kuibuka mshindi baada ya kutuma picha ya chumba chake kilichopambwa na bidhaa alizonunua kutoka katika kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment