Thursday, April 17, 2014

MATUKIO MCHANGANYIKO JIJINI DAR ES SALAAM

Dimbwi kubwa la maji katika maegesho ya kulipia kwa  magari karibu na Ofisi Ndogo ya Bunge Mtaa wa Shaban Robert  Jijini Dar es Salaam je fedha inayopatikana haiwezi kuboresha eneo hilo ?

               Baadhi ya wateja wakiingia na kutoka katika duka la vifaa vya shule na ofisi la Tahfif Mtaa wa Tandamti Kariakoo. Duka hilo huuza vitabu vya vifaa mbalimbali kwa bei rahisi jijini
           Maji ya mvua yakiwa yamejaa katika eneo la ujenzi katika Barabara ya Kawawa Kinondoni Morocco, Dar es Salaam maji hayo yamesababisha kampuni inayojenga barabara hiyo kutumia mashine kunyonya maji hayo ili kuendelea na ujenzi.
                  Duka la Tahfif Kariakoo limekuwa kimbilio kwa watu wenye kipato kidogo ili kujipatia mahitaji kwa ghalama nafuu vifaa vyote vya shule na ofisini vinapatikana hapo.

No comments:

Post a Comment