Tuesday, April 8, 2014

MATUKIO YA MIKOA MBALIMBALI NA NMB BENKI YATIMIZA AHADI KWA WALIMU

  Mkazi wa Wilaya ya Babati,Manyara Bw. Amon Thadeo (kushoto) akishirikiana na Bw. Mohamed bahati kung'oa majani kwenye shamba la mpunga lililopo katika Kijiji cha Mawemairo Magugu, Wialayani Babati, mkoani Manyara (Picha na Mary Margwe)



Mratibu wa Familia 'Kitchen part',  Gala Bi Vida Mndolwa (kushoto) akizungumza  na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu tamasha  la mpango huo linalotegemewa kufanyika kesho Jjumapili katika Ukumbi wa Kilimani Mjini Dodoma.  Kulia  ni Meneja wa Shilika la PSI Tanzania Mkoa wa Dodama ambao ndio washirika wakukubwa wa Mpango huo  ambao pia unatalajia kufanyika Mwanza na Dar es salaam
 Meneja  wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Salie Mlay (kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa kompyuta kwa Mkuu wa Kituo cha  Walimu Wilaya ya Temeke, Daniel Matembele, wakati wa mkutano wao. Huo ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na benki hiyo hinvi karibuni. Katikati ni Ofisa Elimu Temeke Honolina Mumba.
  Meneja wa Tawi la Benki ya NMB Temeke, Harold Lambileki, akikabidhi baadhi ya vifaaa vya ofisi kwa Mkuu wa Kituo cha Walimu Temeke,  Daniel Matembele. (kushoto), wakati wa mkutano wa Walimu Wakuu na Waratibu wa Elimu.
           Baadhi ya maifisa wa benki hiyo wakiwa nje ya ofisi ya Manispaa ya Temeke baada ya kukabidhi misaada.
  Mkuu wa Kituo cha Walimu Temeke, Daniel Matembele (wa pili kulia), akijadiliana jambo na maofisa wa benki hiyo.

No comments:

Post a Comment