|
Mratibu wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la SaHRingo, Martina Kabisama (katikati), akisoma tamko la taasisi hiyo na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dar es Salaam jana, kuhusu ukiukaji wa taratibu za uchaguzi uliojitokeza katika chaguzi ndogo za ubunge hivi karibuni . Kushoto ni Mkuu wa Masuala ya Bunge na Uchaguzi , Hamisi Mkindi na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Dkt. Hellen KMijo-Bisimba. (Picha na Charles Lucas) |
|
Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam akipita kando ya dampo la takatakla lisilo rasmi katika Mtaa wa Swahili, Kariakoo Dar es Salaam jana. Baadhi ya m,awakala waliopewa zabuni za usafi mitaani hawatimizi wajibu huo hali inayohatarisha afya za wananchi. |
|
Mwendesha baiskeli akiinua baada ya kuanguka katika Mtaa wa Mafia Kariakoo Dar es Salaam jana. Baiskeli hiyo ilianguka baada ya kumgonga mama huyo (kushoto) alipofungua mlango wa gari hilo (kushoto) ghafla likiwa barabarani. . |
|
Baadhi ya Askari Polisi na Askari wa Jiji wakiwa katika operesheni ya kuondoa vibanda vya biashara na wafanyabiashara barabarani katika Mtaa wa Nyamwezi Kariakoo, Dar es Salaam jana. Baadhi ya wakazi wa jiji wamepongeza hatua hiyo inayoliweka jiji safi. (Picha na Charles Lucas) |
Moja ya jengo la Mfuko wa Hifadhi ya Mashirika ya Umma (LAPF) lililopo Kijitonyama Mifuko ya jamii imechangia kuliweka jiji katika sura ya kupendeza kutokana na ujenzi wa majengo ya kisasa.
Wateja wa Benki ya
NMB wakipata huduma za kibenki kwenye gari maalumu linalotoa huduma za kibenki
katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, kama walivokutwa na mpiga picha wetu
mwishoni mwa wiki.Gari hilo lina huduma za kuweka na kutoa fedha kama ilivyo
katika matawi mengine ya benki hiyo.
No comments:
Post a Comment