Wednesday, May 7, 2014

DCB BENKI YAELEZEA MAFANIKIO KUELEKEA MKUTANO MKUU 2014 WA MWAKA MEI 24

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Biashara ya DCB Plc ,  Balozi Paul Rupia, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam, kuhusu mafanikio ya benki hiyo kuelekea Mkutano Mkuu wa Mwaka utakaofanyika Mei 24. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Edmund Mkwawa. .

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dr.Charles Kimei akiongea na Waandishi wa habari(Hawapo Pichani) juu ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa benki ya CRDB utakaofanyika hivi karibuni jijini Arusha. Kulia ni Naibu Mkurugenzi  wa Benki hiyo Bi.Esther Kitoka na Mkurugenzi wa tawi la Arusha Bi.Chiku Issa. Benki ya CRDB itafanya mkutano wake Mkuu wa Mwaka tarehe 10/05/2010 katika ukumbi wa AICC jijini Arusha

Wachuuzi wa vinywaji baridi wakijadiliana jambo kuhusu biashara yao na operesheni ya safisha jiji inayoendelea, kama walivyokutwa Mtaa wa Kongo Kariakoo, Dar es Salaam jana. Hali ya usafi jijini imeimarika kufuatia operesheni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB plc, Edmund Mkwawa, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam , kuhusu mafanikio ya benki hiyo kuelekea Mkutano Mkuu wa Mwaka utakaofanyika Mei 24. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Balozi Paul Rupia.

No comments:

Post a Comment