Na Mwandishi maalum
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameunda
Tume ya Uchunguzi (Commission Inquiry)
Kuhusu Vitendo vilivyotokana na Uendeshaji wa Operesheni Tokomeza.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam jion, Ijumaa, Mei 2, 2014 na Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Rais ameunda Tume hiyo kwa mujibu wa kifungu
cha 3 cha Sheria ya Uchunguzi Sura ya 32.
Kutokana
na hatua yake ya kuunda Tume hiyo, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji na
Balozi Mstaafu Hamisi Amiri Msumi kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.
Aidha,
Rais Kikwete amewateua Mheshimiwa Jaji Mstaafu Stephen Ernest Mtashiwa Ihema na
Mheshimiwa Jaji Mstaafu Vincent Kitubio Damian Lyimo kuwa Makamishna. Rais pia
amemteua Ndugu Frederick Manyanda, Wakili wa Serikali katika Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa Katibu wa Tume hiyo.
Taarifa
ya Balozi Sefue imeongeza kuwa uteuzi huu ulianza, Alhamisi, Mei 2014.
No comments:
Post a Comment