Thursday, May 8, 2014

MATUKIO YA KERO MBALIMBALI JIJINI DAR ES SALAAM


Wasamaria wakijaribu kulinasua gari Toyota Landcruser lenye namba SU 36897 lililotumbukia katika mtaro uliofurika maji ya mvua eneo la Gerezani Kariakoo, Dar es Salaam jana. Mitaro mingi katika maeneo mbalimbali haina mifuniko hali inayohatarisha usalama wa watumiaji wa barabara.

Magari yakipita kwa tahadhari kando ya shimo katika Barabara ya Bandari eneo la Gerezani, Dar es Salaam jana. Shimo hilo linalotokana na maji ya mvua linatishia kukata mawasiliano ya Barabara hiyo inayoingia Katika ya jiji na Barabara ya Kilwa.

Baadhi ya mabehewa chakavu yakiwa katika Kalakana ya Shirika la Reli Tanzania katika eneo la Bandari. Mabehewa hayo yachafua mandhari ya eneo hilo ikiwa hayatumiki ni vema yakaondolewa ili kutunza mazingira.

Baadhi ya vibarua wa mawakala wa uzoaji takataka wa Manispaa ya Temeke wakiwa katika dampo lisilo rasmi katika uwanja wa michezo Temeke Mwisho. eneo hilo limegeuzwa dampo hali inayotishia usalama wa afya za wakazi wa eneo hilo.

No comments:

Post a Comment