Monday, May 5, 2014

RUCCO IRINGA MABINGWA WA TAIFA SAFARI LAGER POOL 2014.


Wachezaji wa timu ya Chuo cha RUCCO cha Iringa wakishangilia na kikombe  pamoja na fedha taslimu Shilingi 2,500,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za kitaifa za “Safari Higher Learning Pool Competition 2014” zilizomalizika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.RUCCO waliupata ubingwa huo kwa kukifunga chuo cha St. John 13-12.

Ofisa Tarafa wa Moshi Mjini, William Issa (wa pili kushoto) akimkabidhi kikombe Nahodha wa timu ya Chuo cha RUCCO cha Iringa, Said Mohamed mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za kitaifa za “Safari Higher Learning Pool Competition 2014” zlizomalizika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.Wa pili kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akishangilia na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa, Fred Mushi (kushoto).


Ofisa Tarafa wa Moshi Mjini, William Issa (kushoto) akimkabidhi  Nahodha wa timu ya Chuo cha RUCCO cha Iringa, Said Mohamed kitita cha fedha taslimu Shilingi 2,500,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za kitaifa za “Safari Higher Learning Pool Competition 2014” zlizomalizika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.Kulia ni Betrice Madafu kutoka chuo hicho na katikati ni Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.

No comments:

Post a Comment