Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt Laurent M. Shirima kuwa Mtendaji Mkuu
wa Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA).
Dkt. Shirima
ni Mkurugenzi wa kujenga Uwezo wa Huduma za Ushauri (Capacity Building and
Advisory Service-PPRA) na pia ndiye anaye kaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa
PPRA.
Kulingana na Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Uteuzi huu umeanza tarehe 2 Mei, 2014.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-Dodoma
Tanzania.
6 Mei, 2014
No comments:
Post a Comment