Na Mpigapicha Wetu
Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam jana, kuhusu udhamini wa mashindano ya yanayojulikana kama 'Balimi Ngoma Festival 2014' ya Kampuni ya (TBL). Kushoto ni Meneja Matukio Taifa wa kampuni hiyo, George Mombeki.Na Mwandishi Wetu
KWA mwaka wa 9 sasa Bia ya Balimi Extra Lager imefurahi kutangaza udhamini wake wa Mashindano ya Ngoma za Asili kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa. Mashindano haya yanatarajiwa kuanza Jumamosi Tarehe 7 Juni 2014 na itashirikisha mikoa 6.
Sababu msinigi ya kuwepo kwa Mashindano ya Balimi Ngoma
za Asili ni kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania. Mikoa 6 itakayoshiriki
katika mashindano haya ni: Tabora, Shinyanga, Bukoba, Kahama, Mwanza na Musoma.
Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa katika
mkutano na waandishi wa habari alisema, “Utamaduni ni kitu cha muhimu sana
katika maisha ya binadamu, ni lazima tuenzi na tuzikumbuke. Ni hali ya
kusikitisha pale ambapo watu hawajui tamaduni zao kwani utamaduni unaweza
kutueleza mambo mengi kuhusu vitu ambazo tunanya sasa”.
Finali za kila mkoa zinatarajiwa kuwa kama ifwatavyo:
1. Mkoa wa
Tabora; Jumamosi tarehe 7Juni
2014
2. Mkoa wa
Shinyanga; Jumamosi tarehe 14 Juni2014
3. Mkoa wa
Bukoba; Jumamosi tarehe 21 Juni
2014
4. Mkoa wa
Kahama; Jumamosi tarehe 27
Julai 2014
5. Mkoa wa
Mwanza; Jumamosi tarehe 2 Agosti
2014
6. Mkoa wa
Musoma; Jumamosi tarehe 9 Agosti
2014
7. Mashindano
ya Kanda; Jumamosi tarehe 16
Agosti 2014
Zawadi za kushindania ni:
ZAWADI
|
NGAZI YA MKOA
|
NGAZI YA KANDA
|
Mshindi wa Kwanza
|
600,000
|
1,100,000
|
Mshindi wa Pili
|
500,000
|
850,000
|
Mshindi wa Tatu
|
400,000
|
600,000
|
Mshindi wa Nne
|
300,000
|
500,000
|
Mshindi wa Tano hadi wa Kumi kila kikundi
|
150,000
|
250,000
|
####
Kuhusu TBL
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) ni
watengenezaji na wauzaji wa bia safi, vinywaji vyenye virutubisho na vinywaji
visivyo na kilevi nchini Tanzania. TBL pia ina hisa katika Kampuni ya Tanzania
Distilleries Limited (TDL) na Darbrew Limited.
Vinywaji
maarufu za TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu
Special Malt, Castle Lite, Castle Lager, Castle Milk Stout, Redd’s Original,
Peroni Nastro Azzurro, Balimi Extra Lager, Eagle Lager, Eagle Dark, Club 07,
Vita Malt, Grand Malt and Safari Sparkling Water. Bidhaa nyingine ni Konyagi
Gin na Zanzi Cream Liqueur.
TBL pia imo
katika Soko la Hisa la Dar es Salaam. Imeajiri watu wapatao1, 700 na ina wawakilishi
kote nchini Tanzania ikiwa na viwanda 4 vinavyotengeneza bia safi, kitenge cha
bia ya asili, kiwanda cha kusindika kimea na vitua vya mauzo 10.
No comments:
Post a Comment