 |
Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo, akionesha kwa waandishi wa habari moja ya kupuni zitakazotumiwa na watu mbalimbali kujishindia zawadi mbalimbali katika promosheni inayoendelea ikiwa ni pamoja na safari ya kwenda kuona mechi za Timu ya Barcelona nchini Hispania. Castle Lager pia itaonesha kombe la Dunia kwa kushirikiana na Kituo cha SuperSport. Kulia ni Meneja Masoko la Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Fimbo Butallah. |
 |
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Profesa Joseph Semboja, akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Mwaka wa benki hiyo, uliofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya Wajumbe wa Bodi hiyo na Viongozi wa benki hiyo. |
 |
Meneja wa Zao la Shayiri Dk. Bennie Basson akiwaonesha wakulima kijitabu cha muongozo wa kilimo cha shayiri katikaKijiji cha Emairete Monduli juu, mkoani Arusha juzi. Wakulima hao huwezeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika uzalishaji wa zao hilo ambalo ni malighafi ya kutengenezea bia zinzozalishwa na kampuni hiyo |
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania Kanda ya Mashariki, Julius Nyaga kushoto akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Schalke 04 ya Dodoma, Mussa Gaidi baada ya timu yake kushika nafasi ya kwanza ya Castle Lager Perfect Six kutoka kanda ya Kati katika michezo iliyofanyika uwanja wa Fire Morogoro kwa kukusanya pointi tisa ambapo itawakilisha kanda kwenye ngazi ya taifa kuwania safari ya kwenda Hispania kutembelea uwanja wa Camp Nou na kushuhudia michezo ya klabu ya Barcelona.
No comments:
Post a Comment