Sunday, July 13, 2014

KAMPUNI YA FARM EQUIPMENT (T) LIMITED ILIVYOPAMBA KONGAMANO LA KILIMO MVOMERO


Baadhi ya wakulima waliotembelea banda la Kampuni ya Farm Equip (T) Limited, wakati wa maonesho katika kongamano la mpango wa 'Matokeo Makubwa Sasa BRN' katika kilimo lililofanyika Kijiji chja Mkindo Tuliani mkoani Morogoro juzi, wakiangalia na kusikiliza maelezo kuhusu matumizi ya pambu za kupulizia dawa katika mashamba. Kushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo. Naushad Khan.


Waziri wa Kilimo na Chakula, Mhandisi Christopher Chizza, (kulia juu ya mashine), akifurahi wakati akijaribu kuiendesha mashine ya kisasa ya kuvuna mpunga aina ya Kubota alipotembelea banda la Kampuni ya Farm Equip (T) Limited, wakati wa maonesho katika kongamano la mpango wa 'Matokeo Makubwa Sasa BRN' katika kilimo lililofanyika Kijiji chja Mkindo Tuliani mkoani Morogoro juzi. Chini (Kushoto) ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo. Naushad Khan.
 Baadhi ya wakulima na wakazi wa Mvomero wakiangalia zana za kilimo aina ya Kubota na Sonalika zkatika banda ya la Kampuni ya Farm Equip (T) Limited wakati wa kongamano hilo

Waziri wa Kilimo na Chakula, Mhandisi Christopher Chizza, (katikati), akisikiliza maelezo ya Meneja Mkuu wa Kampuni ya Farm Equip (T) Limited, inayosambaza zana za kilimo nchini, Naushad Khan (kulia), kuhusu matumizi bora ya matrekta ya Kubota na Sonalika yanavyotumika kwa wakulima ili kuunga mkono Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Wakati wa Kongamano lililofanyika Kijiji cha Mkindo Mvomero mkoani Morogoro juzi ambapo mikoa minne ilishiriki. Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ndaki Auto Parts, Iddi Ndaki, ambao ni wasambazaji wa zana hizo mkoani humo.


    Waziri wa Kilimo akiendesha mashine ya kuvuna mazo aina ya Kubota ya Kwenye Banda la Farm Equip (T) Limited

No comments:

Post a Comment