Wednesday, July 9, 2014

MAONESHO YA SABASABA 2014 YALIFANA ZIARA MBILI ZA RAIS KIKWETE ZILIONGEZA MSISIMKO

Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), David Shambwe (kulia), alipotembelea banda la shirika hilo.

Mtawa wa Kanisa Katoliki Parokia ya Ukonga Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Sista Maria (juu ya trekta), akijiandaa kuliendesha trekta aina ya Sonalika, wakati walipotembelea banda la Kampuni ya Farm Equip (T) Limited wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya 38 katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere juzi. Maonesho hayo yalidumu kwa siku 10 yalifungwa rasmi juzi.

Rais Jakaya Kikwete (wa pili kulia), akipunga mkono ikiwa ni ishara ya kuwaaga wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea Maonesho ya 38 ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba), Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara, Jacquline Maleko

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (kulia), akisikiliza maelezo ya  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hiari wa Watumishi wa Umma (PSPF), Adam Mahingu (kushoto) Dar es Salaam juzi, kuhusu mipango ya mfuko huo ukiwamo wa majengo pacha katika picha  (kulia) yanayojengwa eneo la Stesheni Barabara ya Sokoine jijini, alipotembelea banda la mfuko huo katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa (Sabasaba) kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda (kulia), akimkabidhi cheti cha ushindi Ofisa Masoko na Habari wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Lupakisyo Mwasalanga, kwa kutambua mchango wa  na uwezo wa shirika hiyo katika ubunifu na huduma bora, wakati wa ufungaji wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam juzi.

Rais Jakaya Kikwete akiangalia mfumo wa ukusanyaji kodi katika kompyuta, alipotembelea banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wakati wa Maonesho ya 38 ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba), Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Kamishina wa mamlka hiyo, Rished Bade.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia)  akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi, alipotembelea  banda la benki hiyo wakati wa maonesho hayo.



No comments:

Post a Comment