Friday, July 4, 2014

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA YA SABASABA

Baadhi ya wafanyakazi wa  VETA wakiwa na Mkurugenzi Mkuu Zebadiah Moshi (katikati), baada ya kupata tuzo katika maonesho hayo
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi Tanzania (VETA), wakifurahia na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Zebadiah Moshi (kulia) mara baada ya kukabidhiwa ngao na cheti baada ya kupata ushindi wa jumla katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba), Dar es Salaam Jumatano wiki hii.
Mkurugenzi Mkuu  (mwenye suti) kizungumza na baadhi ya watendaji wa VETA
     
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakiangalia vifaa vya kisasa vya kilimo katika banda la Kampuni ya Farm Equip Tanzania Limited, katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba), Dar es Salaam jana. Kampuni hiyo imechangia kuboresha mapinduzi ya kilimo kwa kusambaza zana katika mikoa yote nchini ikiwa ni sehemu ya mkakati wa 'Kilimo Kwanza'
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakiangalia zana za kisasa katika Banda la Kampuni ya FarmEquipment Limited katika maonesho hayo
                                        

Baadhi ya wazazi na watoto wakisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Mauzo wa Benki ya DCB Plc,  Rashid Ngwali (wa pili kulia), kuhusu utaratibu wa kufungua akaunti za watoto, walipotembelea banda benki hiyo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba), Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment