Sunday, March 30, 2014
TANESCO MAGOMENI YACHACHAMALIA WEZI WA UMEME
TANESCO MAGOMENI WACHACHAMALIA WEZI WA UMEME
Umoja matukio.
Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Magomeni imeanzisha opresheni endelevu ya kuwakamata wezi wa umeme na miundombinu ya shirika hilo ili kuboresha huduma za wateja halali
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa operesheni katika maeneo mbalimbali katika mkoa huo Ofisa Usalama wa shirika hilo Mkoa wa Magomeni, Dunia Shami alisema operesheni isiyo na ukomo itafanyika katika mkoa wote ili kuwabaini watu wanaojihusisha na wizi wa umeme na miundombinu yake bila kujali nyadhifa au nafasi yake katika jamii kwa lengo la kukomesha tabia hii. inayolitia hasara shirika.
Ofisa huyo aliongeza kuwa tayari shirika lina taarifa mbalimbali kutoka kwa raia wema wanaoshirikiana kuwabaini wezi hao na mawakala wao hivyo kutokana na tarifa hizo zimesaidia kuwakamata wateja mbalimbali na siku ya jana pekee wateja 9 walibainika kuiba umeme katika maeneo ya Manzese Uzuri, Tandale , Magomeni, Makuburi na maeneo mengine.
'Hatufurahishwi kuwasitishia huduma wateja kwa sababu ambazo wanaweza kuziepoka kwa kufuata utaratibu wa kupata huduma kihalali na kuhoji kwanini ulipie huduma za umeme vichochoroni ikiwa ofisi unazijua ?.' na kuwataka watu wabadilike kwa manufaa yao na shirika
Na kuongeza kuwa shirika limejipanga kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria watu wote watakaokamatwa wakijihusisha na hujuma hiyo na kubainisha kuwa matumizi ya vifaa vya kisasa vya ufuatiliaji wezi wa mita vya GPS utatumika kwa watu waliojifungia mita isivyo halali.
Bi. Shami alisema wateja wote wenye wasiwasi au tatizo linalohusu mwenendo wa matumizi mabaya au yasiyo sahihi ya mita au miundombinu wafike katika ofisi namba 8 na 9 za shirika katika mkoa huo kwa msaada zaidi na kuonya watu wanaowatumia vishoka kupata huduma nje ya shirika kuwa shirika halitatambua huduma iliyotolewa hivyo mteja atakamatwa kama mharifu.
Ofisa huyo alisisitiza wateja kujua haki zao kwa kufika katika ofisi badala ya kupoteza fedha kwa makubaliano ya huduma mitaani hali in ayoweza kuwapotezea fedha na muda na kuongeza kuwa mteja atatakiwa kuwa na stakabadhi halali zitakazomwezesha kutumia huduma husika. vinginevyo utasitishiwa huduma husika mara moja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment