Sunday, March 30, 2014

UZINDUZI KOMBE LA NSSF



Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii inayowahusisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari (NSSF Media Cup) yameanza kutimua vumbi leo katika uwanja wa TCC, Temeke jijini Dar es Salaam.

Mfunguzi wa mashindano hayo, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka, amewataka wanahabari nchini kuhakikisha wanajiunga na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ili kujihakikishia maisha ya amani na utulivu baada ya kustaafu.
Alisema kuwa, wanahabari wanapaswa kwenda mbali zaidi katika kulitumia shirika hilo, ili kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa kwa wanachama.

Katika ufunguzi huo, timu ya soka ya New Habari (2006) Ltd iliumana na Habari Zanzibar katika Soka, ambako hadi  filimbi ya mwisho Habari Zanzibar iliibuka kidedea kwa magoli 4-1, magoli ya Zanzibar yaliwekwa wavuni na Amoor Suleiman aliyeweka wavuni goli moja na Yusuph Juma magoli matatu huku goli la New Habari likiwekwa wavuni na Florian Mwasinde.

Kwa upande wa netiboli, timu ya Jambo Leo iliichapa timu ya Wizara ya Habari Bara kwa jumla ya magoli 59-8, katika pambano la upande mmoja lilipoigwa kwenye viwanja hivyo.
Katika mechi ya pili ya netiboli, Azam Media iliumana na Tanzania Standards Newspaper (TSN), ambako Azam waliibuka washindi kwa magoli 18-13.

Kabaka aliwataka washiriki wa mashindano hayo ya 11 yanayoshirikisha wafanyakazi wa vyombo vya habari kuonesha ushindani, ufundi na nidhamu ili kuongeza hamasa ya michuani hiyo.

Alivitaka vyombo vya habari kuepuka kuingiza wachezaji wasio wanahabari (mamluki), kudumisha lengo la umoja na ushirikiano baina ya shirika hilo kongwe na vyombo vya habari, ikiwamo kuwapa mazoezi wafanyakazi wa vyombo hivyo.

).

No comments:

Post a Comment