Friday, April 11, 2014

KANSA SHINGO YA KIZAZI TISHIO NCHINI




Umojamatukio

IMEELEZWA kuwa Tanzania bado inakabiliwa kwa kiasi kikubwa na ugonjwa  wa kansa ya shingo ya kizazi kwa akina mama ambapo imekuwa > ikisababisha vifo kwa asilimia 37.5 kati ya kila wanawake 100,000.
>
> Kauli hiyo ilitolewa jana na Meneja wa shirika lisilokuwa la  kiserikali la (PSI) linalojihusisha na masuala ya utoaji wa elimu na  huduma za afya nchini Keneth Gondwe, wakati alipokua akizungumza na  waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa Familia Kitchen Part Gala  itakayo fanyika hivi karibuni mjini hapa.
>
> Gondwe alisema kuwa hapa nchini kansa hiyo imekuwa sio tu inayoongoza  katika vifo vya akimama bali pia imekuwa ikikuwa kwa kasi katika nchi  za Afrika ya mashariki.
>
 Aidha alibainisha kuwa katika kuhakikisha kuwa vifo vya akinamama  vinapunguwa PSI wanashirikiana na shirika la Woman in Balance  kuwaletea Familia Kitchen Part Gala itakayo fanyika katika mikoa ya  Dodoma , Mwanza na Dar es Salam.

 Alisema kupitia utalatibu huo wataweza kuwapata akina mama wengi  ambapo pamoja na kuwapatia elimu ya ujasiriamali , saikolojia, na  maisha ya kijamii ili waweze kujitambua pia watawapa elimu katika  suala zima la afya ya uzazi na kanza ya shingo ya kizazi.

 Alisema kuwa Dhima ya ushirikiano huo ni kuhakikisha kuwa vifo vya  akinamama vitokanavyo na uzazi vinakwisha ikiwa ni pamoja na kuwapa  elimu ya uzazi wa mpango pamoja na afya ya kizazi.

 "Tumedhamiria kuhakikisha kuwa Mwanamke anapata ufahamu na elimu  sahihi pamoja na kutoa mwongozo wa wapi pa kupata huduma hizi za uzazi  wa mpango pamoja na upimaji na matibabu ya awali ya kanza ya kizazi" > alisema Gondwe.

 Naye mratibu wa shirika la Woman in balance Vida Mndolwa, alisema kuwa  toka wamenza kufanya utaratibu huo waneshawafikia akina mama zaidi ya  3,000 na kuwapatia mafunzo ya afya uzazi.

 Alisema kuwa pamoja na kuwapatia mafunzo hayo wamekuwa wakiwafuatilia  kwa karibu kuona kama kumekuwepo na madiliko juu ya masuala yote  yanayohusu afya ya uzazi.

 "Mabadiliko yamekuwepo kwa kiasai kikubwa kwa watu ambao wamepatiwa  mafunzo katika utalatibu huu wa Familia Kitchen Part Gala, tofauti na  hapo awali"alisema Mndolwa.

 Hatahivyo alitowa wito kwa kainamama wa mikoa yote ambyo itabahatika  kufikiwa na zoezi hilo kujitokeza kupata elimu pamoja na kucheki afya  zao hasa katika sula la kansa ya shingo ya kizazi amabyo imekuwa  tishio kwao.



KUENDELEA KUKUA KWA TEKNOLOJIA KWATOA FURSA KWA WATANZANIA

Umojamatukio

KUKUA kwa teknolojia ya Mawasiliano ya simu sasa kutawapa fursa Watanzania kupata taarifa za soko za bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo ajira kupitia simu za mkononi kupitia huduma mpya iliyopewa jina la Sokoni.

Kupitia huduma hiyo mteja wa Vodacom aliyejiunga nayo atakuwa na uwezo wa kupokea ama kutoa taarifa za kutaka kununua au kuuza huduma na bidhaa mbalimbali, kutafuta ajira na huduma kupitia simu za mkononi

Bidhaa zinazoweza kuuzwa ama kununuliwa kupitia huduma ya Sokoni ni pamoja na magari, nyumba, mashamba, mitambo n.k huku mahitaji kama vile ajira nayo yakiwezeshwa kupitia pia huduma hii mpya.

Huduma hii ya Sokoni inampa uwezo muuzaji kuweka taarifa ya anachokiuza sanjari na mnunuzi nae kueleza aina ya bidhaa au huduam anayoitafutwa na hatimae kupitia taarifa hizo mteja na mnunuzi au mtafuta huduma na mtoa huduma huunganishw akielektroniki kupitia simu ya mkononi.

Ili kunfaika na huduam hii mteja wa Vodacom anachotakiwa kufanya ni kujiunga kwa kupiga  *149*01*65# katika simu yake ya mkononi na kufuata maelekezo.

“Ni huduma rahisi na rafiki itakayowapunguzia gharama za fedha na wakati wateja wetu kufikia soko iwe kwa kunua au kuuza bidhaa anayoihitaji kwa kuw akwa sasa tumelieleta soko karibu kwenye viaganja vya mikono yao.’ Alisema Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa

“Tumekuwa na shabaha ya kuongeza kasi katika ubunifu na uvumbuzi wa huduma na bidhaa mbalimbali wakati wote ili kuwaptia wateja wetu suluhisho la mahitaji yao na hatiame kuyabadili maisha yao kupitia teknolojia ya simu za mkononi.”Aliongeza Twissa

“Kwa mfano anaetafuta ajira ni rahisi zaidi ya hata kupiga simu au kuperuzi katika mitandao kutafuta matangazo ya nafasi za kazi kwani sasa ni kiasi tu cha kupiga *149*01*65# na kuchagua tafuta ajira na kufuatiwa na maelezo mengine kadiri yatakavyokuwa yakifuata kwenye simu yake ya mkononi.”Alifafanua


Twissa amesema kuongezeka kwa mahitaji miongoni mwa wauzaji na wanunuzi ama watufa ajira na wenye ajira kunatoa changamoto ya kubuniwa kwa mifumo bora yenye uwezo w akutoa taarifa sahihi na za uhakika ili kupunguza pengo baina yao.

“Imezoeleka kuwa mteja na mtoa huduma lazima wakutane mahali ambapo pamezoeleka kujulikana kama soko lakini katika zama za matumizi ya tekonolojia ya habari na mawasiliano ni wazi lazima kuwepo na namna ya kutumia teknolojia katika kupunguza ulazima huo.”Alisema na kuongeza. “Huduma hii ya sokoni inawaketa wauzaji na wanunuzi katika namna rahisi na iliyobora zaidi kuendana na zama tunamoishi”

Amesema pindi mteja atakapojiunga atakuwa akipokea ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu yake ya mkononi hadi mara tatu kwa siku kulingana na mahitaji ya mteja kwa gharama nafuu isiyolinagana na iwapo mteja na mnunuzi huyo wangelazimika kukutana mahali.

Huduma hii inampa nafsi muuzaji kuweka taarifa za aina ya bidhaa ama huduma aitakayo na hivyo kumpa nafasi mnunuzi kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi yanayoendana na mahitaji ayke kwa urahisi zaidi.

No comments:

Post a Comment