Baadhi ya wafanyabiashara ya nguo mbalimbali wakitenganisha nguo hizo kwa madaraja
kulingana na aina ya nguo kabla ya kuwauzia wateja kwa rejareja katika Mtaa wa
Kitumbini, Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Biashara hiyo hufanyika nje ya
maduka kwa makubaliano na wenye maduka.
Baadhi ya mifugo
ikiswagwa kupelekwa katika mnada eneo la Engusero, Kiteto mkoani Manyara, hivi
karibuni eneo hilo lilikumbwa na migogoro ya kugombea ardhi kati ya wafugaji na
wakulima na kusababisha mauaji, hata hivyo mgogoro huo umedhibiwa na Serikali.
|
Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye akiwa na mke wake, Esther akiweka
shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa
mpagania haki za watu weusi, Dkt. Martin Luther King. Wa pili (kushoto)
aliyekuwa Balozi wa Marekani hapa nchini Charles
Stith. |
Mkuu wa wateja
wakubwa wa benki ya NMB,Richard Makungwa akimkabidhi mfano wa hundi Mstahiki
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Didas Massaburi hundi hiyo yenye thamani ya
sh,150,000,000,mkutano mkuu wa 30 wa (ALAT) unadhaminiwa na benki ya hiyo,
utakayofanyika katika Jijini Tanga Mei 7-10 mwaka huu.katikati ni Katibu wa
ALAT Taifa Habraham Shamumoyo.
No comments:
Post a Comment