Sunday, April 6, 2014

SELCOM YAONGEZA AJIRA NCHINI KWA MASHINE ZAIDI 7000 ZA POS


Baadhi ya wayeja wakinunua muda wa maongeze katika Makao Makuu ya Kampuni ya SELCOM Mtaa wa Jamhuri, Posta Dar es Salaam wiki hii. Kampuni hiyo imechangia ajira kutokana na kusambaza mashine zaidi ya 7000 za POS, nchini kote . Kulia ni Ofisa Mauzo Ally Mbaga.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Calderberg, Apollo Temu(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo ya sector ya mafuta na gesi yanayotolewa na kampuni hiyo kwa ushirikiano na kampuni ya Kimataifa ya MDT. Kulia ni Meneja wa MDTI nternational, Douglas Reid.



Mfanyabiashara ya mafuta ya aina mbalimbali wa Engusero, Kiteto mkoani Manyara akimpelekea mteja wake mafuta aina ya petrol yaliyohifadhiwa katika chupa wiki iliyopita. Eneo hilo pamoja na kuwapo kwa mahitaji makubwa ya nishati hiyo hakuna kituo maalumu kinachouza bidhaa hiyo muhimu.



Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mji wa Tunduma, Aidan
Mwanshiga (kushoto) aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya
ya Momba, Abiud Saideya  akimshukuru kwa niaba ya
TBL, Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Claud Chawene
baada ya kukabidhiwa kisima cha maji kilichojengwa
kwa msaada wa kampuni hiyo katika Kituo cha Afya
cha Tunduma. Makabidhiano hayo yaliyofanyika
mwishoni mwa wiki yalikuwa ni moja ya shamra
shamra ya maadhimisho ya Wiki ya Maji.
Baadhi ya wachuuzi wa mahindi mabichi na yaliytochomwa, wakisaka wateja katika magari yaliyokuwa yakisimama katika eneo la Dumila Barabara Kuu ya Dodoma mkoani Morogoro hivi karibuni



No comments:

Post a Comment