Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee David Cleopa Msuya amesema kuwa Rais Kikwete hatasahauliwa kwa kipindi chake cha
uongozi kutokana na upanuzi mkubwa wa shughuli za maendeleo.
Mzee
Msuya ameyasema hayo Aprili 23, 2014 wakati alipozungumza
kuwashukuru na kuwaaga wananchi wa Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro
kufuatia hatua yake ya kunga’atuka katika uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
wilayani humo, shughuli ambayo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete iliyofanyika ofisi za CCM Wilaya
ya Mwanga.
Katika
hotuba yake ndefu, Mheshimiwa Msuya ambaye ameshikilia nyadhifa nyingi za
uongozi nchini ikiwamo ile ya kuwa Mbunge wa Mwanga kwa miaka 20 mfululizo
amemwambia Rais Kikwete:
“Tunakupongeza
kwa kuanzisha uandaaji wa Katiba mpya itakayoongoza Taifa letu la Tanzania kwa
miaka 100 na zaidi ijayo. Zoezi hili likikamilika kama ulivyoliweka
itatuwezesha kusonga mbele na maendeleo ya umma kwa kasi zaidi chini ya utawala
bora unaotabirika. Hii ni shughuli kubwa na muhimu sana kwa
No comments:
Post a Comment