Tuesday, May 13, 2014

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MITAA YA JIJI LA DAR ES SALAAM

         Mkazi wa jiji (jina halikufahamika), alikutwa  'akichakua' katika mapipa ya takataka ili kujipatia vitu vinavyomfaa, kama alivyokutwa Gerezani Kariakoo Dar es Salaam. Tabia hii inaweza kupatwa na magonjwa.
  Askari wa Usalama barabarani akitoa maelekezo kwa madereva wa magari hayo daladala (kushoto) na gari dogo, baada ya kugongana katika makutano ya Barabara za Msimbazi na Uhuru Dar es Salaam.
Askari polisi akizungumza na dereva wa gari hilo baada ya mizigo kuanguka barabara likiwa katika mwendo, eneo la Gerezani Barabara ya Nyerere Dar es Salaam.
Mchuuzi wa mboga za majani na matunda kwenye Soko la Kisutu Dar es Salaam (kushoto), alikutwa akipanga bidhaa hizo kando ya chemba la majitaka lililofunikwa na gurudumu la gari lililokuwa likitoa majitaka .

No comments:

Post a Comment