Thursday, May 22, 2014

MATUKIO MBALIMBALI YENYE MWELEKEO WA KERO JIJINI DAR ES SALAAM

Askari wa usalama barabarani akimuandikia faini dereva wa gari hilo, mara baada ya kukamatwa Shule ya Uhuru Kariakoo, Dar es Salaam.
Mkazi wa jiji mwenye pikipiki akikmaguliwa katika makutano ya Barabara za Lumumba na Nyerere, Dar es Salaam. Hata hivyo ukaguzi huo unapingwa kutokana na kugeuzwa mradi wa wanaosimamia ukaguzi.
Abiria wa pikipiki (kushoto), akisikiliza malumbano kati ya askari wa ulinzi shirikishi na dereva wake, kama walivyokutwa Mnazi Mmoja Dar es Salaam. Wakaguzi hao wamekuwa wakizuia pikipiki zinapokuwa katika mwendo hivyo kuhatarisha maisha.
           Malumbano kati ya mwendesha pikipiki na mkaguzi walipokuwa wakijadiliana jambo kuhusu chombo hicho kuingia katikati ya jiji. Pamoja na kuwa na vibali vinavyotolewa na Manispaa pikipiki zimeendelea kukamatwa.

No comments:

Post a Comment