TAARIFA MAALUMU
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Bw. Gabriel Lyimo Nderumaki kuwa
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali, Tanzania Standard NewsPapers (TSN).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, imesema uteuzi huo umeanza tarehe 19 Mei,
2014.
Kabla ya
uteuzi huo Bw Nderumaki alikuwa Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment