Baadhi ya waumini wa dini hiyo wakiwa katika viwanja vya Kata hiyo wakati wa sherehe za Maulidi zilizohudhuliwa ni Mufti na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Omary Kwang |
Diwani Kariati akipita karibu na vijana walioigiza kama askari wa Mtume Muhammad wakati wa mauliudi hiyo |
Vijana waumini wa Kata hiyo walioigiza kama maswahaba wa Mtume Muhammad (S. A.W), wakiigiza ikiwa ni sehemu ya maulidi hiyo |
Mwandishi Maalumu Kondoa
MUFTI wa Tanzania, Sheikh Issa Shaaban bin Simba, amewaasa viongozi
wa Dini ya Kiislamu, kuwa na umoja na mshikamano ili kuweza
kuhamasisha mema na kukataza mabaya na kuongeza kuwa viongozi wa dini wawe mfano bora wa kuigwa kwa matendo yao.
Akizungumza katika Kata ya Kwadelo na viongozi wa kidini wa kata mbalimbali za Wilaya ya Kondoa, Chemba na Kiteto, mkoani
Dodoma, wakati wa semina ya viongozi hao wa Kiislamu wa kata hizo kiongozi huyo alisema ni wajibu kila kiongozi kuhakikisha kuwa mshikamano na amani inakuwapo katika eneo lake.
"Hakuna Dini ya mtu peke yake hauwezi kuwa Muislam peke yako eti
wewe ujenge Msikiti, Uswalishe huwezi kufika mbali, utapigwa gwala na shetani.' na kuongeza kuwa Mshikamano ni muhimu sana kwa maendeleo kwa kila mmoja wetu nguvu itatokana na umoja huo masheikh kuzungumza na kuongeza ni jambo muhimu linatakiwa kufanywa pia katika familia kwa kuwa umoja ukikosekana malezi ya watoto watayumba na kukosa maadili mema," alisema Mufti.
Kiongozi huyo Mkuu wa Dini ya Kiislamu Nchini ambaye alikuwa katika ziara ya siku tatu, katika wilaya hiyo, alisema iwapo wazee watakuwa hawana
umoja, vijana watakosa maadili kwa sabab=u wazee ndiyo nguzo.
Pia alisema umoja ukikosekana kwa viongozi wa dini ya Kiislamu,
waumini watashindwa kufuata mambo mema. alisema viongozi wa Dini
hiyo wakiwa na umoja wataweza kukataza mabaya na kuimarisha mema.
Mbali na hilo aliwataka waumini wa dini ya kiislamu kuishi kwa taratibu
za dini kwa kufuata yale yote yaliyo mema.
Alisema Uislamu una taratibu zake za kuishi ambazo lazima muumini wa
dini hiyo aufuate Uislamu una taratibu zake za kuishi. Uislamu ni tabia hivyo lazima tuzifuate. Viongozi wa dini lazima tuhakikishe waumini wetu wanaishi kwa kufuata taratibu hizo kwa kuwa bila ya kufanya hivyo vitatoweka.
Aliwaasa viongozi hao kuhakikisha wanawapatia watoto wao elimu za
dini na elimu ya dunia Kwa upande wake
Diwani wa Kata ya Kwadelo, Alhaji Omary Kariati, alisema maagizo ya kiongozi huyo lazima yazingatiwe kwa ustawi wa jamii husika na kuongeza kuwa ustawi wa kisiasa na amani katika jamii na Taifa vinategemea sana maadili mema hivyo wamepokea maagizo ya kiongozi huyo na kuahidi kuyafanyia kazi.
Alhaj Kariati alikiri kwamba uislamu hauwezi kwenda mbele kama
Waislamu wenyewe hawatakuwa na umoja na mshikamano.
"Kauli hii ni kubwa na mzito ambayo tunakuahidi kuichukua na kuifanyia
kazi. Kweli Uislamu hauwezi kwenda mbele kama Waislamu wenyewe
hawataungana na kuusukuma'.
Akiwa katika kata hiyo, Mufti alikuwa mgeni rasmi katika Maulidi,
ambapo alipata fursa ya kuzungumza na waumini wa dini hiyo, ambapo
aliwataka kuwafundisha watoto wao tabia njema ili wawe raia wema na
kuweza kuwasaidia hapo baadaye.
Pia katika mkutano huo uliohudhuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Omary Kwang ilifanyika harambee iliyoendeshwa na diwani huo ya kuchangia fedha za kununua gari la Mufti kwa ajili ya usafiri wake ambapo fedha taslimu zilipatikana sh. 400.000 ahadi sh. milioni 2 na mazao mbalimbali marobota zaidi ya 100.
Mwisho
No comments:
Post a Comment