RAIS Jakaya Kikwete ameondoka Mei 6, 2014 kuelekea Abuja, Nigeria kuhudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum).
Mkutano
huo unaoanza kesho tarehe 7 – 9 Mei, 14, utahudhuriwa na viongozi kutoka Afrika
na duniani kwa ujumla. Pamoja na mambo mengine mkutano utajadili njia
mbalimbali zitakazolifanya Bara la Afrika kuumudu ukuaji wa kiuchumi kwa pamoja
na fursa za ajira zinajitokeza.
Katika
Mkutano huo, viongozi pia watajadiliana jinsi ya kugharamia miundo mbinu Barani
Afrika, njia za kukuza biashara baina ya nchi zao na uwekezaji katika sekta ya kilimo barani
Chini
ya kaulimbiu ya “Forging Inclusive
Growth, Creating Jobs” viongozi pia watajadili kwa pamoja namna ya kukuza
uchumi na uwekezaji kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Wakiwa
Abuja viongozi pia watapata nafasi ya kujadili changamoto zinazolikabili Bara
la Afrika zikiwemo za ukosefu wa ajira, matishio ya kiusalama, vikwazo vya
usafiri barani , upungufu wa chakula na
athari kadhaa za mazingira .
Akiwa
mjini Abuja Rais Kikwete atakutana na viongozi kadhaa wa Afrika na Dunia kwa
ujumla ambao wapo Abuja wakiwemo Waziri Mkuu wa China Bw. Li Keqian , Mjumbe Maalum
wa Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu Bw.
Gordon Brown ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza na viongozi
kadhaa wa mashirika ya kiserikali na kibinafs
No comments:
Post a Comment