TAARIFA MAALUMU
Ni
ugonjwa ambao huwasumbua wakina mama wengi,uvimbe unakuwa kwenye misuli ya
tumbo la uzazi, ama ndani ya tumbo la uzazi.
Ugonjwa
huu kwa kiwango kikubwa huwakumba wakina mama ambao hawaja wahi kuzaa mtoto.
Tafiti
zinaonyeshwa kwamba karibu asilimia 20 ya wana wake wafikapo umri wa miaka 30 wana pata uvimbe kwenye tumbo la
uzazi.kipindi kati ya umri wa miaka 35-45 ni muda ambapo uvimbe hasa
hujitokeza.
Kwa
bahati mbaya kwa walio wengi uvimbe huo hauonyeshi dalili zozte.
Ni
asilimia 3 tu ya wagonjwa wote wenye uvimbe kwenye tumbo la uzazi wanao fika
hospitali wakiwa na dalili.
Chanzo cha uvimbe
Sababu
hasa ya kutokea kwa uvimbe haijulikani.japo sababu zifuatazo zinaweza kuhusika.
a)
Chromosomol abnormality(viini tete kukosa mpangilio wake wa kawaida ama
kutokuwepo kabisa ktk mfumo).Asilimia 40 hupata uvimbe kwa sababu ya chromosormol abnormality
hasa namba sita au saba.
b)
Baadhi ya vichocheo (polypeptide growth factors) ndani ya mwili husababisha
uvimbe kutokea,
kwa
mfano;-Transforming grow factors(TGF), Insulin-like growth factors(IGF).
Ukuaji
Ukuaji
wa uvimbe hutokea hasa kichocheo aina ya oestrogen kinapo kuwa ktk kiwango cha
juu mwilini,ushahidi ni kama ifuatavyo;-
a) Ukuaji wa uvimbe upo tu
kipindi cha uzazi, ambapo kichocheo aina ya oestrogen ipo
kwa kiwango kikubwa.
b) Uvimbe unaongezeka kukua haraka wakati wa
uja uzito,na kwa watumiaji wa vidonge vya uzaji wa mapongo vyenye kiwango
kikubwa cha oestrogen.
c) Uvimbe hautokei kabla ya kuanza hedhi.
d) Baada ya mwanamke kukoma kwenda
hedhi,uvimbe hukoma kukua pia hakuna uvimbe mpya unao jitokeza.
Uvimbe
kwenye tumbo la uzazi unaweza kuwa sehemu moja ama sehemu mbalimbali kwa
wakati mmoja.(multiple)
Wakati
mwingine uvimbe hukuwa haraka haraka ama hukuwa taratibu.
Dalili
Asilimia
75 ya wagonjwa wenye uvimbe kwenye tumbo la uzazi hawaonyeshi dalili yeyote ,kwa
bahati njema uvimbe hugundulika wakati daktari anapomfanyia mgonjwa uchunguzi.
Mahali
uvimbe ulipo ktk tumbo la uzazi ni muhimu sana kuliko ukubwa wa uvimbe wenyewe.
A) Mabadiliko ktk hedhi (ni dalili
muhimu kwa wagonjwa wenye uvimbe kwenye tumbo la uzazi)
1. Utokaji wa damu unaongezeka kwa mfuatono
kila mzunguko wa mwezi unaofuata.
kwa
sababu zifuatazo;-
i)Uvimbe unazuia /unaharibu upanukaji wa
tumbo la uzazi wakati wa hedhi..
ii)Uvimbe unaongeza ukubwa wa nafasi ndani
ya tumbo la uzazi.
iii)Kunatokea msongamano /mkusanyiko wa damu
ktk baadhi ya sehemu za uzazi kwa sababu
uvimbe kuziba baadhi ya njia za damu.
2.
Utokaji wa hedhi usio na mpangilio.
B Kupata maumivu wakati wa hedhi.
C)
Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.
D)
Ugumba.(infertility)
E)
Kuharibika kwa mimba.(Abortion)
D)
Maumivu ya tumbo chini ya kitovu.
F)
Kuongezeka ukubwa wa tumbo.
Uchunguzi ama Njia za kugundua uvimbe kwenye tumbo la
uzazi.
i)
Kupiga ultra soundi ya
tumbo.
Na vipimo
vingine kadri dackari atakavyo ona inafaa.
No comments:
Post a Comment